MATAYARISHO YA 2022

Masahibu wa karibu: Naibu rais William Ruto atembelea Museveni ikuluni mwake, Entebbe

Mwaka wa 2019 rais Museveni aliagiza chuo kikuu cha Makerere kujenga taasisi ya uongozi wa William Ruto ndani ya chuo hicho

Muhtasari

•Kulingana na ujumbe na picha iliyochapishwa na Museveni kwenye mtandao wa Twitter, wawili hao walionekena kuwa kwa majadiliaono ingawa haikuelezwa wazi walichokuwa wakizungumzia.

•Museveni alimwalika Ruto kama mgeni mkuu kwenye hafla ya kuzindua ujenzi wa kiwanda cha kutengenezea madawa ya kibiolojia na chanjo ya mRNA kilicho eneo la Matugga, Uganda siku ya Jumanne.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakizungumza na naibu rais William Ruto katika ikulu ya Uganda jijini Entebbe, July 8
Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakizungumza na naibu rais William Ruto katika ikulu ya Uganda jijini Entebbe, July 8
Image: TWITTER// YOWERI MUSEVENI

Naibu rais Wiiliam Ruto ambaye ako katika ziara nchini Uganda alimtembelea mwandani wake, rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda katika ikulu yake jijini Entebbe, Uganda.

Kulingana na ujumbe na picha iliyochapishwa na Museveni kwenye mtandao wa Twitter, wawili hao walionekena kuwa kwa majadiliaono ingawa haikuelezwa wazi walichokuwa wakizungumzia.

"Naibu rais wa Kenya William Ruto alinitembelea kiheshima ikuluni, Entebbe jioni ya leo katika" Museveni aliandika.

Kwa muda sasa wawili hao wameonekana kuwa marafiki wa dhati huku ikidhaniwa kuwa huenda  kiongozi wa Uganda kwa miaka 35 ni mshauri wa naibu rais.

Museveni alimwalika Ruto kama mgeni mkuu kwenye hafla ya kuzindua ujenzi wa kiwanda cha kutengenezea madawa ya kibiolojia na chanjo ya mRNA kilicho eneo la Matugga, Uganda siku ya Jumanne.

Ruto alisema kuwa wanatazamia kujumuisha mataifa ya bara Afrika ili kuweza kutengeza madawa badala tu ya kuzifunga zinapowasiri kutoka ughaibuni.

"Tuko makini kujenga ushirikiano baina ya mataifa ya Afrika ili kusonga kutoka kupanga na kuandika dawa tu na kuweza kuzitengeneza. Ununuzi wa dawa zilizotengenezewa Afrika utawezesha kupunguza ada ya kuagiza bidhaa kutoka nje na kuleta mapato ya kuuza bidhaa nje na kuimarisha afya ya Waafrika" Ruto alisema kupitia akaunti yake ya Twitter.

Mwaka wa 2019 rais Museveni aliagiza chuo kikuu cha Makerere kujenga taasisi ya uongozi wa William Ruto ndani ya chuo hicho. Ruto alizindua taasisi hiyo mwezi wa Desemba mwaka huo.