'Nataka kumwambia ajisalimishe,'Wazazi wa askari muuaji hatimaye wazungumza

Muhtasari
  • Wazazi wa askari muuaji hatimaye wazungumza
Mshukiwa wa mauji ya watu wawili Caroline Kangogo
Mshukiwa wa mauji ya watu wawili Caroline Kangogo
Image: HISANI

Maafisa wa DCI wamekuwa wakimsaka afisa wa polisi wa kike Caroline Kangogo ambaye anaonekana kuwa kwenye msururu wa mauaji.

Vitengo kadhaa vya polisi vimewekwa katika hali ya tahadhari kumsaka afisa wa polisi Caroline Kangogo, mtuhumiwa wa mauaji ya Konstebo wa Polisi John Ogweno, huko Nakuru.

Hatua ya kuhusisha vikosi zaidi vya polisi kumsaka mshukiwa ilitokana na tukio la pili ambapo afisa huyo anashukiwa kumpiga risasi tena mtu mwingine eno la Juja, karibu kilomita 200 kutoka tukio la kwanza. Jamaa aliyeuawa alitambuliwa kama Peter Ndwiga Njiru, 32.

Caroline amegongwa vichwa vya habari kwa muda sasa, huku wazazi wake wakizunumza wakati wa maombi nyumbani mwao Elgeyo Marakwet baba yake alimsishi mwanawe ajisalimishe kwa polisi kwani anafahamu sheria vyema.

"Nataka kumsihi mwanangu ajisalimishe kwa polisi kwa maana pia naye ni polisi na anajua sheria

Anapaswa kujisalimisha na kuoea serikali silaha," Aliongea Barnaba Kibor.

Mama yake Leah Kangogo ambaye alionekana kusikitishwa na tabia za mwanawe alishindwa na jinsi mwanawe alibadilika licha yake kuwa mzuri na msaidizi katika familia.

"Mtoto wangu haukufanya vyema kuua watu, unapaswa kuja na kusema kama kuna shida,pole kwa familia ya watu ambao waliuawa na mtoto wangu

Ni kifungua mimba wangu na sijui kwanini amebadilika,anapenda watu sana na nimeshtuka tena sana alikuwa anakuja nyumbani," Alisema Leah.