Viongozi wenzangu tuwache kusumbua rais-DP Ruto

Muhtasari
  • Naibu Rais William Ruto amewashambulia viongozi wa National Super Alliance, na kuwaambia wampe Rais Uhuru Kenyatta muda wa kufanya kazi kwa Wakenya
William Ruto
William Ruto
Image: Hisani

Naibu Rais William Ruto amewashambulia viongozi wa National Super Alliance, na kuwaambia wampe Rais Uhuru Kenyatta muda wa kufanya kazi kwa Wakenya.

Akiongea huko Huruma ambapo alihudhuria ibada ya kanisa katika African Holy Ghost Christian Church Jumapili, Ruto alisema kuwa Rais alichaguliwa kuhudumia Wakenya zaidi ya milioni 45 na watu wachache tu.

"Haiwezekani kwa miaka nne watu watano wanasumbua Rais tubadilishe katiba kwa sababu ya tamaa yao ya kupata vyeo,"Ruto Aliongea.

Kigogo huyo aliwatuhumu  viongozi wa Nasa  kwa kubadilisha mwelekeo wa Mkuu wa Nchi kuwaunganisha kwa sababu hawawezi kukubaliana kati yao, baada ya juhudi za kubadilisha katiba kutupiliwa mbali.

Korti ya Rufaa bado haijatoa uamuzi juu ya rufaa ya mchakato wa BBI ambayo ilisikilizwa na benchi saba la majaji.

"Viongozi wenzangu tuwache kusumbua rais amechaguliwa kupanga maendeleo ya wakenya zaidi ya milioni arobaini na tano hajachaguliwa kuhudumia watu watano wa upande hio ingine."