Jamaa ajitia kitanzi baada ya kukatazwa kuuza shamba ya familia Muhoroni

Familia ya marehemu ilikuwa imekutana mapema siku ile ili kujaribu kutafuta suluhu ya mzozo uliokuwa ila maafikiano hayakupatikana.

Muhtasari

•Joseph Odhiambo Ouma, 23, anaripotiwa kujitia kitanzi akiwa kwa  nyumba ya jirani kufuatia uamuzi huo wa familia.

•Mwili wake ulipatikana Jumapili jioni ukiwa umening'inia kwa nyumba ya jirani ambako alikuwa anafanya kazi kama msimamizi wa nyumba.

WXvImZ-B.jfif
WXvImZ-B.jfif

Mwanaume mmoja kutoka Muhoroni  alijitoa uhai siku ya Jumapili baada ya ndugu zake kumzuia kuuza shamba la familia ili kupata leseni ya gari.

Joseph Odhiambo Ouma, 23, anaripotiwa kujitia kitanzi akiwa kwa  nyumba ya jirani kufuatia uamuzi huo wa familia.

Kulingana na kamanda wa kaunti ya Kisumu Samuel Anampiu, familia ya marehemu ilikuwa imekutana mapema siku ile ili kujaribu kutafuta suluhu ya mzozo uliokuwa ila maafikiano hayakupatikana.

Baada ya juhudi za kutafuta maafikiano kugonga mwamba Ouma alitishia kujitoa uhai.

"Aliskika akisema kuwa anaenda kujitoa uhai kwa sababu ndugu zake wamemnyima haki yake ya uridhi" Anampiu alisema.

Mwili wake ulipatikana Jumapili jioni ukiwa umening'inia kwa nyumba ya jirani ambako alikuwa anafanya kazi kama msimamizi wa nyumba.

Upelelezi kuhusiana na kifo hicho umeanza huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika mochari ya Ahero.