Raila Odinga aomboleza kifo cha Mke wa Mweka Hazina wa Chama cha ODM

Muhtasari
  • Raila Odinga aomboleza kifo cha Mke wa Mweka Hazina wa Chama cha ODM
KInara wa ODM Raila Odinga
Image: Maktaba

Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga ameomboleza kifo cha mke wa mbunge wa zamani Timothy Bosire, Jane Bosire.

Katika taarifa, kiongozi huyo wa ODM aliomba faraja ya Mungu kwa familia ya familia ya aliyekuwa mbunge wa Kitutu Masaba.

"Mama Ida na mimi tunatuma pole zetu za dhati na za dhati kwa Mhe. @TimothyMEBosire kufuatia kufariki kwa mke wako mpendwa Jane Bosire. Kama familia na kama ODM tunasimama nawe wakati huu mgumu. Uko katika maombi yetu. Tunamwomba Mungu Mwenyezi atawapa nguvu, "Raila alisema.

Marehemu alikata roho akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi, haijabainika alikuwa akiugua ugonjwa upi lakini inasemekana amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu.

Kifo chake kilitangazwa kupitia mitandao ya kijamii na chama cha ODM Jumanne, Julai 21.

" Tumehuzunishwa na kifo cha Mama Jane Bosire, mke wa mweka hazina wetu Mheshimiwa Timothy Bosire. Marehemu aliaga dunia Jumanne, Julai 20 akipokea matibabu katika hospitali ya Nairobi. Kama chama tutasimama na familia ya mheshimiwa wakati huu wa huzuni na majonzi na tuomba Mungu aifariji," ODM ilisema.