Kutupiana maneno haitatuletea suluhu,Wacheni kunitusi mkiwa jukwaani-Uhuru

Muhtasari
  • Rais Uhuru Kenyatta amewauliza viongozi kujizuia wasimtukane wakiwa jukwaani wakati wakijipigia debe
Rais Uhuru Kenyatta
Image: PSCU

Rais Uhuru Kenyatta amewauliza viongozi kujizuia wasimtukane wakiwa jukwaani wakati wakijipigia debe.

"Njoo tuketi tukazungumze ... usinitupie matusi kwenye jukwaa mahali pengine. Pale ambapo wazee wameketi, kutakuwa na suluhisho kila wakati," alisema.

Uhuru alikuwa akizungumza wakati alikuwa akitoa hati miliki katika kaunti ya Kilifi Alhamisi.

"Kutupiana maneno haitatuletea suluhu, nikukuja pamoja,Hapa tumeketi sijali kama mtu ni wa chama tofauti. Hakuli ODM sikuli Jubilee, sote tunakula jasho ya kazi tunayofanya. Wale hawataki watu wawe pamoja, hawana suluhu ya shida

Lazima tutafute barabara itakayohakikisha waKenya wanaletwa pamoja na sio kutenganishwa."

Uhuru aliendelea kusema kuwa wale waliopewa hati miliki wanapaswa kuhakikisha wanapata utajiri kutoka kwake.

"Mtu kuwa na title deed ya anakoishi yaleta mambo mengi kwa kuwa ni mwisho wa ufukara kwasababu mtu anajua anakoishi, kesho hataharakishwa, na jina squatter ianze kutoka kwa midomo yetu. Tuko hapa (pwani) kupatiana vyeti vya hatimiliki karibu 2,169 

Umepata cheti chako cha ardhi, pesa iko mikononi mwako; hiyo pesa kupitia cheti chako utatumia kuimarisha maisha yako ama utaenda barabarani uuze na kufikia Desemba mjamaa hana chochote? Mhifadhi vyeti vya ardhi,"

Pia rais aliwaambia watu wa Kilifi kwamba wanapaswa kupitisha mchakato wa BBI kwani utawasaidia wananchi.