Majambazi 2 wauawa, 4 watoroka na majeraha kwenye makabiliano ya risasi na polisi Eastleigh

Tanki mbili za maji walizokuwa wanajaribu kupakia kwa gari lao baada ya kuziiba zilirejeshwa dukani

Muhtasari

•Kulingana na DCI, genge la wezi sita waliokuwa wamejihami kwa bunduki walivamia duka la kuuza vifaa la Jamarat na  kujaribu kuiba wakati maafisa wa polisi walifika na kuzuia uhalifu kuendelea.

•Wawili wao waliaga papo hapo kutokana na majeraha huku wengine wakinusurika kifo na majeraha ya risai mwilini.

Crime scene
Crime scene

Majambazi wawili waliokuwa wamejihami waliuliwa na wengine wanne kutoroka na majeraha ya risasi walipokabiliwa na polisi kwenye jaribio la wizi maeneo ya Eastleigh.

Kulingana na DCI, genge la wezi sita waliokuwa wamejihami kwa bunduki walivamia duka la kuuza vifaa la Jamarat na  kujaribu kuiba wakati maafisa wa polisi walifika na kuzuia uhalifu kuendelea.

Katika harakati ya kujaribu kujinusuru kifungo majambazi hao walikabiliana na maafisa hao kwenye vita ya risasi ila  wakawezwa nguvu. 

Wawili wao waliaga papo hapo kutokana na majeraha huku wengine wakinusurika kifo na majeraha ya risai mwilini.

Bastola iliyokuwa na risasi tatu na chuma ya kung'oa misumari ni baadhi ya vitu vilivyopatikana katika eneo la tukio.

Tanki mbili za maji walizokuwa  wanajaribu kupakia kwa gari lao  baada ya kuziiba zilirejeshwa dukani.