Wavuvi wawili waliozama ndani ya ziwa Victoria baada ya kupata mabomu sita wako salama-DCI

Muhtasari
  • Wavuvi wawili waliozama ndani ya ziwa Victoria baada ya kupata mabomu sita wako salama
Image: DCI

Kundi la wavuvi waliokuwa wakivua samaki katika ziwa Victoria walipigwa na butwaa baada ya kuvua sanduku kubwa la chuma lililokuwa na mabomu sita badala ya samaki.

Wavuvi hao kutoka mji wa Mbita magharibi mwa Kenya waliodhani wamepata samaki mkubwa asubuhi ya Jumatatno, walikimbilia kufungua sanduku hilo lakini walipata mambomo yenye kutu.

Wawili kati ya wavuvi hao walipiga mbizi kwenye ziwa hilo kwa kuhofia mabomu hayo huenda yakalipuka huku wenzao watatu wakati wakiongoza boti ufuoni.

Mkurugenzi wa DCI George Kinoti alisema wavuvi hao wawili walijiunga na wenzao katika Ufukwe wa Litare katika Kisiwa cha Rusinga Alhamisi.

"Wawili hao wamesimulia jinsi walivyogelea kwa kasi kwenda Kisiwa cha Rabuor kwa usalama bila kujua hatari waliyojiweka," Kinoti alisema.

Kupitia mitandao ya kijamii, Kinoti alisema wavuvi walisema kuwa wako hai kwa ustadi wao wa kuogelea.

Mnamo mwaka wa 2019 mabomu yaliyosadikiwa kutoka enzi ya ukoloni yalipatikana yamefichwa kwenye sanduku la zamani la mbao ndani ya ziwa.