logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu 4 wakamatwa baada ya kunaswa na polisi wakiiba kutoka kwa lori lililosheheni mizigo ya milioni 1.8

Pia katika eneo la tukio, polisi hao walipata koti la polisi.

image
na Radio Jambo

Habari31 August 2021 - 08:26

Muhtasari


  • Watu wanne wamekamatwa baada ya kunaswa na polisi wakiiba kutoka kwa lori lililosheheni fimbo za chuma zenye thamani ya Sh1.8 milioni huko Kendu Bay, Kaunti ya Homa Bay

Watu wanne wamekamatwa baada ya kunaswa na polisi wakiiba kutoka kwa lori lililosheheni fimbo za chuma zenye thamani ya Sh1.8 milioni huko Kendu Bay, Kaunti ya Homa Bay.

Polisi walisema lori hilo lilikuwa limetumwa kutoka Kampuni ya Chuma ya Abyssian Iron and Steel na ilikuwa ikielekea Kisii wakati tukio hilo linatokea.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, alikuwa akifuatilia mzigo huo, alishuku baada ya lori hiyo kubadili njia  kutoka  iliyotengwa kufikia Oyugis na kuelekea Kendu Bay.

Kulingana na Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), maafisa walinasa lori katika eneo la Rakwaro Kamwala, ambapo lilikuwa limesimama na viboko vya chuma vilikuwa vimeshushwa.

"Alipowaona maafisa wa polisi, mmoja wa majambazi aliyevaa mavazi ya polisi aliwafyatulia risasi maafisa hao alipotoweka gizani, kuelekea mwambao mwa Ziwa Victoria," DCI alisema .

Maafisa hao, walifanikiwa kuwakamata  washukiwa waliotambuliwa kama Byron Apollo Ochieng, John Omondi Ochieng, Bernard Otieno Owuor na Quinter Otieno katika eneo la tukio na kuwasindikiza hadi kituo cha Polisi cha Kendu Bay kwa mahojiano.

Pia katika eneo la tukio, polisi hao walipata koti la polisi.

"Wapelelezi wanachunguza ikiwa nyaraka zilizopatikana ni za kweli na ikiwa zinaweza kuhusishwa na mtuhumiwa mwenye silaha aliyekimbia eneo la tukio," DCI aliongeza.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved