Bunduki iliyotumika katika eneo la tukio la mauaji ya vijana wanne Kitengela yapatikana

Muhtasari

•Mashahidi kadhaa wamedai kuwa mwanaume mmoja alipiga risasi moja hewani ili kuzuia mauaji ya wanne hao ila hakuna muuaji aliyetishika.

Picha ya Bunduki
Picha ya Bunduki
Image: HISANI

Wapelelezi wanaochunguza mauaji ya vijana wanne maeneo ya Kitengela mnamo Agosti 8 wamepata bunduki iliyotumika kupiga risasi katika eneo la tukio.

Kamanda wa polisi katika kaunti ya Kajiado Muthuri Mwongera amesema kuwa bunduki ile haikutumika kutekeleza mauaji laikini inatuhumiwa kutumika kupiga risasi katika eneo la tukio.

Hata hivyo Mwongera hakufichua wakati bunduki hiyo ilipatikana.

"Tuko na bunduki hiyo na wapelelezi wanafuatilia. Huenda tukaweza kukamata washukiwa wengine" Mwongera alisema siku ya Jumanne.

Mwongera alisema kuwa kesi ile sio rahisi na kudai kuwa wapelelezi wanafaa kupewa muda ile wachunguze kwa umakini na kuhakikissha kuwa wanaokamatwa walihusika kwenye mauaji.

Alisema kuwa polisi wanachunguza madai kuwa kulikuwa na magari 16 kwenye eneo la tukio muda mfupi kabla ya vijana wale wanne kuuawa.

Mashahidi kadhaa wamedai kuwa mwanaume mmoja alipiga risasi moja hewani ili kuzuia mauaji ya wanne hao ila hakuna muuaji aliyetishika.

Inadaiwa kuwa jamaa aliyepiga risasi hewani alienda kwa gari lake na kuondoka baada ya wauaji wale  kufanya maamuzi ya kumalizia kazi yao.

(Utafsiri: Samuel Maina)