'Tutarudi tena tuongee zaidi,'Raila asema baada ya kukaribishwa kwa shangwe Kiambu

Muhtasari
  • Raila Odinga akaribishwa kwa shangwe Kiambu
Raila Odinga akihutubia wakazi wa Kiambu
Image: Twitter/Raila Odinga

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga alipkewa kwa shangwe na wakazi wa kaunti ya KIambu baada ya kuhudhuria mazishi ya Grace Muthoni Mungai yaliyofanyika Ngecha, Kiambu. 

Raila alisema yeye amekuwa rafiki wa kweli wa eneo la Mlima Kenya akisema alileta mswada wa BBI ili kusaidia eneo hilo.

Huku akizungumzia suala la mchakato wa BBI Raila alisema kuwa;

"Kuleta BBI haikuwa kwa sababu ya Raila au Uhuru, ilikuwa ya kutatua shida tulizoona. Kwa mfano tuligunua hakuna haki katika ugavi wa rasmali, . . . kuna kaunti zingine ziko na watu 800K na wanapata bilioni 12 huku Kiambu ikiwa na watu milioni mbili unusu inapata bilioni tisa, hio si haki," alisema Raila.

Raila pia alimshambulia DP Ruto na kampeni yake ya 'kazi ni kazi' akisema huu si wakati wa vijana kupewa toroli.

Hata hivyo kupitia kwenye ukurasa wake wa twitter Raila aliahidi wakazi wa kiambu kwamba atarudi tena wazungumze zaidi.

"Leo hii tumehudhuria mazishi ya mama Grace Muthoni Mungai yaliyofanyika Ngecha, Kiambu.

Baadaye, tuliwasalimia wakazi wa eneo hilo waliokiri kwamba wanaunga mkono Azimio la Umoja.

Tutarudi tena tuongee zaidi," Aliandika Raila.