Wakenya wanaweza kuwa wamesahau kisa hicho na kuendelea na maisha yao, lakini uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi.
Ni takriban miezi miwili tangu ndugu 2 wa Kianjokoma kaunti ya Kiambu kudaiwa kuuawa na polisi masaa ya kafyu.
Emanuel na Benson walikuwa wakitoka kazini kuelekea nyumbani walipokutana na mauti yao.
Mama yao Catherine Wawira, akiwa kwenye mahojiano na TV47, alisema kwamba tangu wanawe waage dunia hajakuwa na nguvu ya kukutana na watu.
"Tangu watoto wangu waage dunia sijawahi wala kusikia kuenda sokoni wala kuhudhuria vyama, lakini tunaachia Mungu
Benson alikuwa anapenda mambo ya upishi, naye ndugu yake alikuwa anapenda ukulima, alikuwa na kuku ambao nilikuwa nawalinda, ni ndugu ambao walikuwa na furaha sana," Alizungumza Catherine.
Kulingana na Catherine walikuwa wamepangana na mume wake wazae watoto wanne, huku akisema hata akiamua kuzaa hawezi kujifungua wanawe ambao waliaga dunia.
"Ata ukiamua kujifungua siwezi jifungua Benson ama Emanuel, huwa napita kwenye vyumba vyao vya kulala kila asubuhi na kutandika vitanda vyao hivi ndivyo huwa nakutana na wanangu ata kama hawayuko."
Catherine anatarajia kupata haki kwa wanawe.