Gavana Waiguru atangaza kutetea kiti chake 2022 kupitia chama cha UDA

Muhtasari
  • Gavana Waiguru atangaza kutetea kiti chake 2022 kupitia chama cha UDA
Gavana Waiguru akizungumza mwakani 2019
Gavana Waiguru akizungumza mwakani 2019
Image: Hisani

Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru ametoa dalili ya wazi kuwa atatetea kiti chake cha ugavana na tiketi ya chama cha UDA.

Akizungumza na wakazi wa Kirinyaga Jumatano, Waiguru alitangaza nia ya kulinda kiti chake.

Alionekana kukubaliana na wito wao ili kulinda kiti chake kwenye tiketi ya UDA.

Waiguru alikuwa amewaomba umati kama wangeweza kumchagua kama Gavana na waliitikia kwa uthibitisho.

“Nilisema nitafanya vile watu wa Kirinyaga wanataka. Nataka niwaulize mnataka nikuje na chama gani huku Kirinyaga ili mnirudishe? Waiguru aliuliza.

“Nikikuja na hio chama mtanirudisha? Mimi nitasema si mimi nilisema, nimeuliza wananchi na nitafanya vile wanasema,” alisema Waiguru baada ya kuarifiwa ajiunge na UDA.