Chifu asingiziwa madai ya ubakaji na mke wa wenyewe ambaye wamekuwa wakifanya ngono naye shambani Kericho baada ya kufumaniwa

Muhtasari

•Inaripotiwa kwamba mwanadada huyo aliponaswa na mumewe aliandamana naye hadi kituo cha polisi na kuandikisha ripoti kuwa chifu wa eneo hilo alikuwa ameenda nyumbani kwao mapema siku hiyo na kumuamuru atoke nje kisha akamlazimisha amfuate hadi kwa shamba la mahindi lililokuwa karibu ambapo alimbaka

•Ilibainika kwamba wawili hao wamekuwa wakiandikiana jumbe tamu  za mapenzi na kukutana mara kwa mara katika shamba la mahindi ambalo walikuwa wamegeuza kuwa kitanda cha ndoa.

crime scene
crime scene

Mwanamke mmoja kutoka eneo la Kimasian, kaunti ya Kericho anaaminika kutoa madai ya uwongo dhidi ya chifu wa eneo kwamba alimlazimisha kushiriki tendo la ndoa naye. 

Kulingana na DCI, Mercy aliandamana na mumewe ambaye ni mwendeshaji bodaboda kupiga hadi kituo cha polisi cha Londiani siku ya Jumanne ili kushtaki chifu huyo kwa kosa la ubakaji. 

Mercy alimshutumu chifu kwa kosa la ubakaji baada ya mumewe  kugundua kuwa wawili hao wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Inaripotiwa kwamba mwanadada huyo aliponaswa na mumewe aliandamana naye hadi kituo cha polisi na kuandikisha ripoti kuwa chifu wa eneo hilo alikuwa ameenda nyumbani kwao mapema siku hiyo na kumuamuru atoke nje kisha akamlazimisha amfuate hadi kwa shamba la mahindi lililokuwa karibu ambapo alimbaka.

Kufuatia madai hayo chifu yule alikamatwa na kuzuiliwa huku uchunguzi zaidi uking'oa nanga.

Uchunguzi wa kina ambao ulifanywa na wapelelezi kutoka kituo cha  Londiani ulibaini kwamba kulikuwa na uhusiano wa kimapenzi kati ya Mercy na mshtakiwa ambao ulikuwepo  kwa kipindi kirefu.

Ilibainika kwamba wawili hao wamekuwa wakiandikiana jumbe tamu  za mapenzi na kukutana mara kwa mara katika shamba la mahindi ambalo walikuwa wamegeuza kuwa kitanda cha ndoa.

Mnamo siku ya Jumapili mshtakiwa alikuwa amemtumia Mercy ujumbe uliosoma "Tupatane hapo kwa mahindi yenu".

Ujumbe mwingine ambao ulitumwa siku ya Jumanne ulisoma "nimekuwekea kitu tupatane nikupatie..". Hii ilikuwa  baada ya chifu kumtumia Mercy shilingi 327.

Jumbe hizo za simu kati ya chifu na Mercy zilifanya mumewe agundue kwamba wawili hao wamekuwa wakijiburudisha pamoja shambani. Kufuatia ugunduzi huo Mercy alilazimika kumshtaki chifu yule ila uchunguzi zaidi ukathibitisha kwamba madai yale yalikuwa ya uongo.

Wapelelzi waliweza kupata jumbe za Mpesa zilizoashiria kwamba mwanadada yule alikuwa akitumiwa pesa na chifu mara kwa mara.

Ilibainika kwamba mumewe Mercy alikuwa amewekea chifu yule mtego kwa kumuambia wapatane na mkewe.

Baada ya uchunguzi kukamilika imebainika kwamba madai dhidi ya chifu yule yalikuwa ya uongo na ukweli ni kwamba wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi tangu mwezi Agosti.

Kufuatia hayo  raia wameonywa dhidi ya kushtaki wengine kwa madai ya uongo kama njia ya kulipiza kisasi.