Linturi ameomba upande wa mashtaka kuachilia Sh200,000 alizompa mwanamke katika kesi ya kujaribu kumbaka

Muhtasari
  • Linturi ameomba upande wa mashtaka kuachilia Sh200,000 alizompa mwanamke katika kesi ya kujaribu kumbaka
Seneta wa Meru Mithika Linturi
Seneta wa Meru Mithika Linturi
Image: ENOS TECHE

Seneta wa Meru Mithika Linturi mnamo Jumanne aliambia mahakama ya Nairobi kwamba anataka upande wa mashtaka uachilie Sh200, 000 zake ambazo alimpa mwanamke anayedaiwa kujaribu kumbaka.

Seneta Linturi anashtakiwa kwa kujipenyeza kwenye kitanda cha chumba cha hoteli cha mwanamke na kujaribu kumbaka huko Nanyuki.

Kesi hiyo ilipotajwa Jumanne kabla ya kusikilizwa, Seneta huyo kupitia kwa wakili wake Muthomi Thiankolu alimweleza hakimu wa mahakama ya Milimani Susan Shitubi kwamba upande wa mashtaka unafaa kuachilia pesa zake zilikuwa na mlalamishi.

Thiankolu alisema serikali imekuwa ikishikilia kwa mwaka mmoja uliopita.

“Heshima yako natoa maombi ya kutaka upande wa mashtaka uachilie Sh200,000 ambazo wanazimiliki kwa mwaka mmoja uliopita, fedha hizo ni za mteja wangu na zilichukuliwa na mlalamikaji na polisi,” alisema wakili huyo.

Wakili huyo pia aliiomba mahakama iamuru serikali impatie maelezo ya shahidi wa mlalamikaji na OB wakidai kuwa hawakuwa kwenye orodha ya maelezo na maandishi aliyokabidhiwa.

Akijibu, wakili wa upande wa mashtaka Alice Mathangani aliambia mahakama kwamba afisa anayechunguza kesi hiyo anahitaji muda ili kuthibitisha kama nyaraka hizo ziko mikononi mwake na kuziwasilisha kwa timu ya utetezi.

Alice pia aliambia mahakama kwamba Sh200,000 ambazo Linturi anataka mwendesha mashtaka arejee kwake ni kielelezo kitakachotumika mahakamani kama ushahidi wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo. hivyo haiwezi kuachiliwa hadi itakapowasilishwa mahakamani.

Katika shtaka hilo, Linturi anadaiwa kuwa mnamo Januari 30, 2021, mwendo wa saa tisa asubuhi katika hoteli ya Maiyan Villas huko Nanyuki, kwa makusudi na isivyo halali alijaribu kumbaka mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36.

Anakabiliwa na kosa lingine la kumgusa mwanamke huyo bila ridhaa yake.

Seneta huyo alikanusha mashtaka na yuko nje kwa dhamana ya pesa taslimu Sh200,000.

Hakimu Mashauri aliamuru shauri hilo litajwe baada ya wiki mbili ili kuthibitisha utoaji wa nyaraka zote kwa upande wa utetezi.