Wazazi wa Shule ya Upili ya Kakamega kulipa Sh21.6m kukarabati bweni lililoteketea kwa moto

Muhtasari
  • Katika barua kwa wazazi wote ya Novemba 11, Sh21, 611,350 ziliafikiwa baada ya kikao cha bodi mnamo Novemba 10
Moto mkubwa
Moto mkubwa
Image: WIKIPEDIA

Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Kakamega watalipa jumla ya Sh21.6 milioni kukarabati uharibifu uliotokea mnamo Novemba 6 wa moto ulioteketeza bweni.

Katika barua kwa wazazi wote ya Novemba 11, Sh21, 611,350 ziliafikiwa baada ya kikao cha bodi mnamo Novemba 10.

Kulingana na usimamizi wa shule, uharibifu halisi kulingana na tathmini ya Wizara ya Uchukuzi, Miundombinu na Makazi ni Sh12.1 milioni.

Uongozi pia ulichangia Sh695,420 kwa gharama ya ufungaji wa CCTV katika bweni ambalo bado halijajengwa, na vitanda 280 vya ghorofa mbili vikiwa Sh4.1 milioni na kufikisha Sh21.6 milioni.

Kila mmoja wa wanafunzi 2,200 ameagizwa kulipa Shilingi 9,823 siku ya kuripoti ili kukarabati bweni.

Kundi la kwanza la wanafunzi linatarajiwa kurudi Jumatatu, Novemba 15.

"Jumla ya uharibifu ni Sh21.6 milioni, ikigawanywa na wanafunzi 2,200, kila mwanafunzi atalipa Sh9,832," ilisema barua hiyo.

Wazazi pia wameagizwa kumaliza ada zote ambazo hazijalipwa za Muhula wa Pili.