Rais Uhuru aomboleza rais wa zamani wa Afrika Kusini FW de Klerk

Muhtasari
  • Klerk alikuwa mkuu wa nchi kati ya Septemba 1989 na Mei 1994
  • Alikuwa rais wa mwisho mweupe wa Afrika Kusini
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Frederik Willem de Klerk.
Image: Hisani

Rais Uhuru Kenyatta Ijumaa alifariji Afrika Kusini kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais Frederik Willem de Klerk.

Katika ujumbe wake, Uhuru alimkumbuka Klerk kwa kuwa na jukumu muhimu katika kuhakikisha nchi inapita bila ubaguzi wa rangi hadi demokrasia.

Alikuwa rais wa mwisho mweupe wa Afrika Kusini.

"Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa rambirambi na faraja kwa Rais @CyrilRamaphosa na watu wa Jamhuri ya Afrika Kusini kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Nchi hiyo Frederik Willem de Klerk," taarifa kutoka Ikulu ilisema.

Klerk alikuwa mkuu wa nchi kati ya Septemba 1989 na Mei 1994.

Kifo chake kilitangazwa Alhamisi, Novemba 11.

“Bw de Klerk, 85, aliwahi kuwa Mkuu wa Serikali ya Afrika Kusini kati ya 1989 na 1994, na alichangia pakubwa katika kipindi cha mpito cha demokrasia kutoka kwa utawala wa kibaguzi nchini humo, jambo ambalo lilimletea Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1993 pamoja na Rais wa zamani Nelson Mandela. "

Hata hivyo, jukumu lake katika kipindi cha mpito kuelekea demokrasia lilipingwa sana. Mwaka jana, alijiingiza katika mzozo uliofanya ashtumiwe kwa kudharau uzito wa ubaguzi wa rangi. Baadaye aliomba radhi kwa "kubisha" juu ya suala hilo.