Hatuko tayari kuwazuia Wakenya kustarehe, tunatafuta tu wadanganyifu wa ushuru - KRA

Muhtasari
  • Wiki iliyopita Mburu aliwamulika sosholaiti  akisema wataangalia mtindo wao wa maisha ama unalingana na ushuru wao

Hatuko tayari kuwazuia Wakenya kustarehe, kamishna mkuu wa KRA Githii Mburu amesema.

Wiki iliyopita Mburu aliwamulika sosholaiti  akisema wataangalia mtindo wao wa maisha ama unalingana na ushuru wao.

Akiongea na Hot 96 Jumanne, Mburu alisema wanachotafuta kutoka kwa mtandao wa kijamii ni udanganyifu wa ushuru.

"Hatuko tayari kuwazuia Wakenya kustarehe. Kwa kweli tunaunga mkono watu wanaofanya vizuri kwa hivyo endeleeni kufurahia... tunatafuta tu wadanganyifu wa ushuru," alisema.

"Ninataka Wakenya wajue kuwa sisi ni washirika na tunawatakia walipe ushuru Tunalenga tu kuhakikisha kwamba unalipa sehemu yako halali ya ushuru."

Alisema wanafuatilia miamala ya watu wanaojihusisha na biashara zenye shaka na utakatishaji fedha ambao ni maarufu kwa jina la ‘wash wash’.

“Sisi pia tuko kwenye shingo ya hata hawa watu wa ‘wash wash’,” Mburu alisema.

Aliwataka Wakenya kulipa ushuru akisema hiyo ndiyo njia pekee ya serikali kufadhili hospitali, kulipa maafisa wa usalama na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Mnamo Novemba 8, KRA ilisema itaanza kuangalia ikiwa mitindo ya maisha ya watu inalingana na ushuru wao.

"Katika mitandao ya kijamii, tuna watu wengine wanaotuma vitu vizuri. Ungeona wengine wakiweka viatu vizuri, nyumba nzuri, magari yanayopeleka familia zao mahali pazuri,” Mburu alisema.

Tangazo hilo lilizua mjadala mkali ambao ulishuhudia watumiaji wa mitandao ya kijamii wakiigeuza kuwa meme, ikionyesha jinsi mtoza ushuru angezunguka kukusanya ushuru, na jinsi Wakenya wangeitikia.

Naibu Kamishna wa KRA anayesimamia Masoko na Mawasiliano Grace Wandera baadaye alisema KRA inatumia kikamilifu suluhu za kiteknolojia, zikiwemo zana za ufuatiliaji wa mitandao ya kijamii.

Aliwapongeza Wakenya kwenye Twitter (KoT) miongoni mwa wabunifu wengine wa maudhui mtandaoni kwa kubuni maudhui ya kuvutia kuhusu ushirikiano wa KRA na walipa ushuru.

Wandera alibainisha kuwa machapisho hayo;

Ongezeko hilo ni la kupongezwa kwani inamaanisha walipa ushuru wako tayari kufuata, na KRA iko karibu kutoa usaidizi unaohitajika," Wandera alisema.