Msanii Rufftone kuwania kiti cha useneta wa Nairobi mwaka ujao

Muhtasari
  • Msanii Rufftone kuwania kiti cha useneta wa Nairobi mwaka ujao
Msanii Rufftone
Image: Hisani

Roy Smith Mwita almaarufu Rufftone, mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za Injili nchini , amefichua kwa mara ya kwanza kwamba anapanga kuwania kiti cha useneta wa Nairobi katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.

"Ninafichua hili kwa mara ya kwanza kuhusiana na mustakabali wa Rufftone. Unamtazama Seneta mpya wa Nairobi anayekuja

I will be vying in 2022, mimi sisikie ground, Naambie ground," Alisema Rufftone.

Kwa tamko hilo, Rufftone sasa amejiunga na orodha inayokua ya watu mashuhuri ambao wametangaza nia ya kuwania  viti  tofautivya kisiasa mwaka wa 2022.

Subscribe NOW to Churchill Show to watch the latest videos: http://bit.ly/1TQQNWo Connect with us on - FACEBOOK: https://www.facebook.com/mwalimchurchill/ https://www.facebook.com/ChurchillTVKenya/ TWITTER: https://twitter.com/Churchill_Show https://twitter.com/MwalimChurchill INSTAGRAM: https://www.instagram.com/mwalimchurchill/ Churchill Show 2021 #ChurchillShow

Kabla ya kuingia kwenye siasa, mwanamuziki huyo alisema kuwa atakuwa akifanya, Ziara za vyuo vikuu kote nchini, zikitoa mfano wa athari za Covid kwenye tasnia ya muziki.

Mwimbaji huyo wa nyimbo za injili alisema kuwa lengo lake na ziara za chuo kikuu ni kuwashauri wanafunzi wachanga na kwamba matukio kiingilio ni bila malipo yanalenga kukuza amani kupitia sanaa.