logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tamasha la Koffi Olomide lasitishwa Kenya

Hatua hiyo inakuja wakati ambao mwanamuziki huyo alipotumbuiza katika mji mkuu wa Kigali wa Rwanda.

image
na Radio Jambo

Habari06 December 2021 - 08:52

Muhtasari


  • Hatua hiyo inakuja wakati ambao mwanamuziki huyo alipotumbuiza katika mji mkuu wa Kigali wa Rwanda
editor594634055701458020

Tamasha la mwanamuziki nyota barani Afrika Koffi Olomide, lililotarajiwa kufanyika Desemba 11, jijini Nairobi limekatishwa baada ya mwanamuziki huyo kutumbuiza nchini Rwanda.

Waandalizi wa tamasha la Kenya wameahidi kurejesha pesa kamili kwa mashabiki waliopata tiketi za onyesho hilo, wakitaja sababu kadhaa za kuhairishwa kwa tamasha hilo.

Hatua hiyo inakuja wakati ambao mwanamuziki huyo alipotumbuiza katika mji mkuu wa Kigali wa Rwanda.

Huku wanaharakati waliomba onyesho hilo lisiendelee kutokana na sifa yake ya kuwanyanyasa wanawake.

Mnamo mwaka wa 2019, mwimbaji huyo wa Soukus wa Kongo ambaye jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba alipatikana na hatia ya ubakaji wa kisheria wa mmoja wa wachezaji wake wa zamani wakati binti hyou akiwa na umri wa miaka 15.

Olomidé alishtakiwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2012 kwa ubakaji lakini mashtaka yalipunguzwa.

Amekuwa matatani na sheria mara kadhaa hapo awali kwa kumvamia mmoja wa wachezaji wake, mpiga picha na mtayarishaji wake.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved