Basi na magari mawili madogo yahusika katika ajali ya barabarani Vihiga

Muhtasari

•Wakati wa tukio hilo basi la Modern Coast na moja ya magari ya saloon yaliteketea na kuwa majivu.

Hakuna majeruhi aliyeripotiwa kutokana na ajali hiyo iliyohusisha Basi la Modern Coast na magari mawili ya saloon.
Hakuna majeruhi aliyeripotiwa kutokana na ajali hiyo iliyohusisha Basi la Modern Coast na magari mawili ya saloon.
Image: MARTIN OMBIMA

Magari matatu yalihusika katika ajali ya kugongana uso kwa uso siku ya Jumatatu katika eneo la hoteli ya Bendera, kando ya Barabara kuu ya Kapsabet-Chavakali.

Alipokuwa anathibitisha ajali hiyo, Kamanda wa polisi kaunti ya Vihiga Benjamin Ong'ombe alisema  magari hayo matatu yalikuwa Saloon mbili na basi moja.

""Tunafurahia kuona kuwa hakuna walioangamia katika ajali hiyo," Ong'ombe alisema

“Dereva wa basi lililokuwa likielekea Kapsabet alijaribu kukwepa magari mawili ya saloon yaliyokuwa yamehusika katika ajali ndogo,” Ong’ombe aieleza.

"Katika harakati hizo, matairi ya basi yalipasuka na kuwaka moto."

Aliongeza kuwa bado wanaendelea na uchunguzi kuhuu masuala mengine ambayo huenda yalisababisha kuzuka kwa moto huo kwenye basi hilo

Kamanda huyo ametoa wito kwa madereva wa magari binafsi na ya umma kuwa makini ila kuepukana na ajali katika msimu huu wa sikukuu.

Wakati wa tukio hilo basi la Modern Coast na moja ya magari ya saloon yaliteketea na kuwa majivu.

Abiria waliokuwa ndani ya gari hilo walilazimika kutoka nje ya gari kwa ajili ya usalama wao wakati wa ajali hiyo.

(Utafsiri: Samuel Maina)