Arsenal yashtakiwa na shirikisho la soka FA

Muhtasari
  • Tukio hilo lilitokea dakika ya 59 baada ya beki wa Gunners, Gabriel kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupokea kadi ya pili ya njano

Klabu ya Arsenal imeshtakiwa na Shirikisho la soka Uingereza FA kwa kushindwa kuhakikisha wachezaji wao wanajiendesha kwa utaratibu ufaao wakati wa mechi ya Jumamosi dhidi ya Manchester City.

Tukio hilo lilitokea dakika ya 59 baada ya beki wa Gunners, Gabriel kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupokea kadi ya pili ya njano.

Arsenal wana hadi Januari 7 kujibu

KWINGINEKO NI KUWA;

KFC yaahidi kununua viazi vya Kenya baada ya malalamiko

Kampuni ya vyakula ya KFC, imewaahidi wateja wa Kenya kwamba itavinunua viazi vya nchini humo kufuatia lalama kwamba huwa inaagiza viazo kutoka nje.

Migahawa yake nchini Kenya ilikuwa imeacha kutoa vibanzi au chipsi kwa sababu ya changamoto za usafirishaji zilizosababishwa na Covid.

Lakini Wakenya walieleza kuwa wakulima wa eneo hilo walikuwa na akiba ya kutosha ya viazi.

Baadhi kwenye mitandao ya kijamii walitaka KFC isusiwe, wakihoji ni kwa nini ilihitaji kuleta viazi hivyo kutoka Misri.

Mwakilishi wa kampuni hiyo alisema wasambazaji walilazimika kupitia uhakikisho wa ubora.

KFC ndio kampuni ya hivi punde zaidi kukumbwa na usumbufu wa Covid.