logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu wakamatwa kwa kupanda bangi katika ofisi ya rais

Kiongozi wao, ambaye hujiita Mfalme wa Khoisan, alianguka ndani ya mmea wa bangi wakati polisi walipokuwa wakimburuza kumlazimisha atoke wamkamate na kumpeleka kituo cha polisi.

image
na Radio Jambo

Habari13 January 2022 - 08:01

Muhtasari


  • • Mimea hiyo ni mali ya wanaharakati kutoka jamii ya wazawa ya Khoisan, ambao baadhi yao wamekita kambi katika eneo hilo kwa kipindi cha miaka mitatu.
AFP

Mfalme wa Khoisan wa Afrika Kusini  akamatwa kwa kupanda bangi katika ofisi ya rais.

Mimea hiyo ni mali ya wanaharakati kutoka jamii ya wazawa ya Khoisan, ambao baadhi yao wamekita kambi katika eneo hilo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kiongozi wao, ambaye hujiita Mfalme wa Khoisan, alianguka ndani ya mmea wa bangi wakati polisi walipokuwa wakimburuza kumlazimisha atoke wamkamate na kumpeleka kituo cha polisi.

"Polisi ... mmetangaza vita?," shirika la habari la AFP lilimnukuu Mfalme wa Khoisan akipaza sauti akisema.

"Tumekuwa hapa kwa amani. Tunawajia," aliendelea. Baada ya matamshi hayo alikamatwa.

Yeye na baadhi ya wanaharakati waliokamatwa kwa "kuhusika na dagga (bangi), upandaji na uvunaji haramu wa bangi na kukataa kuvaa barakoa wanapokuwa katika maeneo ya umma wakati walipoamrishwa na afisa wa polisi kufanya hivyo," taarifa ya AFP ilisema.

Mnamo mwaka 2018, kikundi hicho kiliweka kambi yao katika eneo la bustani nje ya ofisi ya rais, karibu na sanamu kubwa ya Nelson Mandela, kufanya kampeni ya kutambuliwa rasmi kwa lugha yao.

Mke wa Mfalme wa Khoisan ameelezea kukasirishwa kwake na tukio hilo katika mahojiano na wavuti wa habari wa Afrika Kusini wa IOL.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved