Ngilu amtetea Kalonzo, amtaka Ruto akome kuwatusi viongozi

Muhtasari
  • Kupitia kwenye ukuraa wake wa Facebook Jumamosi, Ngilu alisema hawatamruhusu Ruto kuja Ukambani na kumtusi kiongozi wao mwadilifu
Gavana wa Kitui Charity Ngilu
Image: Musembi Nzengu

DP William Ruto anafaa kuacha kuwatusi viongozi, gavana wa Kitui Charity Ngilu amesema.

Ngilu alikuwa akirejelea matamshi ya Ruto kuwa kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka amepoteza nywele kwa kumuunga mkono kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga.

“Ruto anafaa kuacha kuwatusi viongozi na maeneo ambayo viongozi hao wanatoka,” Ngilu alisema.

Kupitia kwenye ukuraa wake wa Facebook Jumamosi, Ngilu alisema hawatamruhusu Ruto kuja Ukambani na kumtusi kiongozi wao mwadilifu.

"...kama vile alivyofanya huko Meru akiwa na Gavana Kiraitu Murungi tukitazama. Haitajirudia," alisema.

"Ajiangalie, tofauti ya umri kati yao ieleweke kuwa hatakiwi kumtukana Kalonzo ambaye amekuwa uongozini kwa muda mrefu."

Ngilu alisema tofauti kati ya viongozi hao wawili ni kwamba Kalonzo ni mwaminifu na mtu mwingine sio.

"Kalonzo anategemewa sana na amejitahidi sana kuleta amani, ukimlinganisha yeye na Ruto ni kama usiku na mchana. Kalonzo anajaribiwa, sio jina la kucheza nalo. Huwezi kuja Ukambani kuongea vibaya. ya mtu wa Kalonzo," alisema.

Wiki iliyopita, Ruto alimweleza Kalonzo.

"Mimi sina shida na mtu yeyote, nilisaida Raila hadi akawa Waziri Mkuu lakini ilifika wakati nikagundua hapendi Mungu nikachoka nikamwachia Kalonzo," alisema.