Harambee stars itakuwa kwenye Afcon ijayo-Raila Odinga aahidi

Muhtasari
  • Raila alisema iwapo atachaguliwa kuwa rais, serikali yake itawekeza katika soka
  • Raila alikuwa akizungumza baada ya Sadio Mane kufunga mkwaju wa penalti wa ushindi wakati Senegal ikinyakua taji la kwanza kabisa la Kombe la Mataifa ya Afrika
Raila Odinga akabidhiwa viatu vya kukwea Mlima na viongozi wa Murang'a
Raila Odinga akabidhiwa viatu vya kukwea Mlima na viongozi wa Murang'a
Image: SABINA CHEGE FOUNDATION

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga ameahidi kuhakikisha Harambee Stars inashiriki Kombe la Mataifa ya Afrika iwapo atachaguliwa kuwa rais mnamo Agosti 9.

Raila alikuwa akizungumza baada ya Sadio Mane kufunga mkwaju wa penalti wa ushindi wakati Senegal ikinyakua taji la kwanza kabisa la Kombe la Mataifa ya Afrika kwa ushindi wa 4-2 kwa mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya washindi mara saba wa Misri kufuatia sare ya 0-0 katika mchezo wa kuamua mjini Yaounde Jumapili.

"Hongera Senegal kwa kushinda. Ninaahidi kikosi cha mashabiki wa soka wa Kenya kuwa chini ya utawala wangu, Harambee stars itakuwa kwenye Afcon ijayo," Raila alisema.

Jumapili jioni, kupitia ukurasa wake wa Twitter, Raila alisema iwapo atachaguliwa kuwa rais, serikali yake itawekeza katika soka.

"Tutawekeza kwenye soka kwa kuanzia na klabu za msingi/mtaani na jumuiya," alisema.

Kurejea kwa Harambee Star kwenye Afcon baada ya kusitishwa kwa miaka 16 kuligubikwa na madai ya ubadhirifu mkubwa wa fedha zilizotolewa na serikali kuelekea kampeni nzima.

Jaribio la Kenya kujitokeza nchini Cameroon liliingia dosari, kufuatia msururu mbaya wa mchujo, ambapo walichapisha matokeo mseto na kumaliza nafasi ya tatu nyuma ya Misri na Comoro.

Harambee Stars ilishinda mechi ya pekee pekee, huku ikitoa sare nne na kupoteza katika mechi nyinginezo.