logo

NOW ON AIR

Listen in Live

NMS kutupa miili iliyokosa kuchukuliwa na familia kwenye hifadhi za maiti

NMS inatafuta amri ya kutupa miili iliyokosa kuchukuliwa na wapendwa wao.

image
na Davis Ojiambo

Habari04 March 2022 - 08:22

Muhtasari


  • • Shirika la ustawishaji wa jiji la Nairobi NMS sasa linapanga kupata  amri ya kutupa miili ya watu 132 katika hifadhi za maiti mbalimbali mjini Nairobi, ambao haijachukuliwa na familia zao .
  • • Miili 32 ipo katika hifadhi ya maiti ya Mama Lucy, 8 kati yao ikiwa ya wanawake huku 24 wakiwa wanaume, kati ya miaka 15-73.
Mkurugenzi wa NMS Meja jenerali Mohamed Badi

Shirika la ustawishaji wa jiji la Nairobi NMS sasa linapanga kupata  amri ya kutupa miili ya watu 132 katika hifadhi za maiti mbalimbali mjini Nairobi, ambao haijachukuliwa na familia zao .

Kupitia notisi iliyotolewa na NMS tarehe 4/3/2022, mkurugenzi wa huduma za matibabu ndani ya NMS, Ouma Oluga alisema shirika hilo litatafuta amri ya kutupa miili hiyo iwapo haitachukuliwa siku saba baada ya notisi hiyo kutolewa.

“Kwa mujibu wa sheria ya afya ya umma ibara  ya 242, familia za marehemu waliotajwa humu wanapaswa kuichukua miili ya wapendwa wao ndani ya siku saba, la sivyo NMS itaomba amri ya kutitupa miili hiyo,” Oluga alisema. 

Miili 32 ipo katika hifadhi ya maiti ya Mama Lucy, 8 kati yao ikiwa ya wanawake huku 24 wakiwa wanaume, kati ya miaka 15-73.

NMS imefanikiwa kutambua miili yote kupitia alama ya vidole  ila saba ambao bado hawajatambulika. Sita kati yao ni wanaume huku mmoja akiwa mwanamke.

Katika hifadhi ya maiti ya City, miili 139 bado haijachukuliwa. Kulingana na ripoti, idadi kubwa ya watu hao waliaga kutokana na ajali za barabarani, kujitia kitanzi, vifo vya ghafla, kupigwa na umma, kunywa sumu na vifo vya kawaida.

Mara ya mwisho kwa NMS kutafuta amri ya kutupa miili iliyokosa kuchukuliwa na familia zao ilikuwa ni Oktoba 2021.

Kipindi hicho, miili 164 ilikuwa haijachukuliwa katika hifadhi mbalimbali za maiti. .

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved