Nina hakika angetaka viongozi wetu wamwache Mungu awe midomoni mwao-Askofu Muheria

Muhtasari
  • Askofu Muheria awashauri wanasiasa,huku akimuomboleza Kibaki
Image: ENOS TECHE

Marehemu Rais mstaafu Mwai Kibaki hatawahi kuwasema vibaya washindani wake wakati wowote, Askofu Mkuu wa Nyeri Anthony Muheria aliwaambia waombolezaji wakati wa ibada ya maziko ya marehemu Mwai KIbaki.

Alipokuwa akiongoza hafla ya maziko yake katika shule ya Othaya Approved, Muheria aliwataka waombolezaji waliokuwepo na Wakenya kwa ujumla kujiruhusu kuwa wabebaji wa rehema za Mungu jinsi Kibaki alivyokuwa.

Aliongeza kuwa Kibaki angetaka viongozi wa Kenya wakome kushabikia matamshi ya chuki na badala yake wahubiri amani.

"Nina hakika angetaka viongozi wetu wamwachie Mungu midomoni mwao. Tunahitaji kisafishaji maalum ili kuua vinywa vyetu vyenye sumu."

Askofu Mkuu kiongozi aliwataka Wakenya na viongozi kuacha kuchukiana.

Alisema Kibaki anapenda amani na angetamani nchi isalie katika hali ya amani.

Pia alisema kuwa Kibaki alikuwa mtu ambaye hatawahi kutumia uwongo kujinufaisha binafsi.

Muheria aliwataka Wakenya kuwa wakweli kila wakati kama heshima kwa kiongozi huyo aliyeanguka.

"Tuwe wakweli na tuwe wakweli bila kuoneana jeuri."

Muheria aliongeza kuwa Kibaki alikuwa mtu asiye na ubinafsi na 'aliyejituma' ambaye alitumikia Wakenya kwa uadilifu.

"Hakuwahi kukosea. Leo angetuambia tuwapende kaka na dada zetu," Muheria alisema.

Muheria zaidi aliwataka Wakenya na viongozi kuwa wanyenyekevu kama Kibaki.

"Tudumishe imani. Inamaanisha pia unyenyekevu na hilo ni jambo moja tunaweza kuiga kutoka kwa baba yetu Kibaki. Leo ni mfano wa kutaka kuzikwa kwa urahisi," alisema.

Askofu Muheria aliipongeza familia ya Kibaki kwa kufuata nyayo zake za unyenyekevu.

Mtu wa Mungu alikumbuka wakati ambapo Kibaki alizuru kanisa kuu la Nyeri katika uzee wake na kupiga magoti kuungama na baada ya hapo, alitoka kimyakimya bila kugeuza kanisa kuwa uwanja wa kisiasa wenye ghasia.