DP Ruto,Raila wawasherehekea wafanyikazi sikukuu ya leba

Muhtasari
  • DP Ruto,Raila wawasheherekea wafanyikazi sikukuu ya leba

Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wamewaenzi wafanyikazi wa Kenya wakiadhimisha sherehe za siku ya Wafanyakazi kote nchini.

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuongoza sherehe hizo katika uwanja wa Nyayo Jumapili hii.

Katika ujumbe wake, Ruto alikiri jukumu muhimu ambalo wafanyikazi wa Kenya wameathiri uchumi akisema wameifanya nchi kuwa kama ilivyo.

"Kwa wafanyikazi na hustlers Tunatambua taabu yenu, jasho na bidii yenu. Ninyi ndio sababu ya kwamba Kenya iko wapi na ilivyo leo. Ninyi ndio injini ya kutufikisha huko. Mungu awabariki," alisema.

Kupitia kwenye ukurasa rasmi wa twitter kinara wa ODM aliwaahidi wafanyikazi malipo sawa katika utawala wake endapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi wa Agosti 9.

"Taifa sio kitu bila wafanyakazi wanaohisi kuridhika, usalama na kuthaminiwa. Utawala wa Azimio utahakikisha kuwa Wakenya wote watapata malipo ya kutosha kwa juhudi zao za kuhakikisha utu wao unadumishwa. Heri ya Siku ya Wafanyakazi," Raila alisema.

Kutoka kwetu wanajambo tunawatakia wafanyikazi wote sikukuu njema ya leba.