Mwanamke na mwanawe mchanga wavamiwa na kuuawa na mbwa wa kasisi, Siaya

Muhtasari

•Mbwa hao wanaripotiwa kuwa wa kasisi mmoja wa Kikatoliki aliyetambulishwa kama  Felix Omach.

•Mbwa hao walikuwa na njaa kufuatia kutokuwepo kwa mmiliki wao na walitoka nje ya banda lao Jumapili usiku.

Mbwa wanaodaiwa kuwavamia na kumuua mwanamke na mtoto wake mchanga huko Siranga, kaunti ya Siaya, baada ya kuuawa na wanakijiji.
Mbwa wanaodaiwa kuwavamia na kumuua mwanamke na mtoto wake mchanga huko Siranga, kaunti ya Siaya, baada ya kuuawa na wanakijiji.
Image: JOSIAH ODANGA

Mwanamke mmoja na mwanawe waliuawa na mbwa wawili katika eneo la Simur, kaunti ndogo ya Ugenya.waliotoka kwenye kibanda chao katika kitongoji cha Simur katika kaunti ndogo ya Ugenya.

Caren Akinyi Aluoch, 28, na mwanawe wa mwaka mmoja waliuawa na mbwa hao ambao walikuwa wamevunja banda lao na kutoka nje.

Tukio hilo lilitokea Jumatatu katika Kituo cha Biashara cha Siranga. Kufuatia hayo wanakijiji waliokuwa wamejawa na ghadhabu waliwapiga mbwa hao hadi kifo.

Mbwa hao wanaripotiwa kuwa wa kasisi mmoja wa Kikatoliki aliyetambulishwa kama  Felix Omach.

Haikujulikana mara moja aliko kasisi huyo na inasemekana alienda DRC alikokuwa akifanya kazi. Polisi walikuwa wakimtafuta.

Mbwa hao walikuwa na njaa kufuatia kutokuwepo kwa mmiliki wao. Walitoka nje ya banda lao Jumapili usiku.

Mkazi mmoja alisema mwanamke aliyeuawa alikuwa na mazoea ya kuamka mapema sana na kutembea barabarani.

Naibu OCPD wa Ugenya James Ngao alithibitisha kisa hicho. "Msimamizi wa nyumba aliripoti kwamba mbwa walikuwa wametoka nje ya boma. Mwanamke na mtoto wake walipatikana Jumatatu asubuhi wakiwa wamekuliwa na mbwa hao wakatili,” Ngao alisema.

Miili ya mwanamke huyo na mwanawe ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya kaunti ndogo ya Ukwala.