logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mhubiri akataa kutoka jela licha ya kuachiliwa huru

Mahakama ilimwachilia ikisema kuwa serikali imeshindwa kuthibitisha kesi yake.

image
na Samuel Maina

Habari06 May 2022 - 11:13

Muhtasari


  • •Sheikh Guyo Gorsa Buru alikamatwa Januari 2018 kaskazini mwa Kenya na kushtakiwa kwa kushirikiana na kundi la wanamgambo wa al-Shabab.
  • •Bw Buru amewasilisha kesi tofauti katika mahakama kuu akitaka kupata ulinzi wa serikali pindi atakapoachiliwa.
Picha ya gereza ya Kamiti

Kiongozi wa dini ya Kiislamu ameiomba mahakama ya Kenya kutomwachilia huru licha ya kuachiliwa kwa makosa ya ugaidi.

Sheikh Guyo Gorsa Buru alikamatwa Januari 2018 kaskazini mwa Kenya na kushtakiwa kwa kuwa na nyenzo za kulitangaza kundi la kigaidi na kwa kushirikiana na kundi la wanamgambo wa al-Shabab.

Lakini wiki hii, mahakama ilimwachilia ikisema kuwa serikali imeshindwa kuthibitisha kesi yake.

Hata hivyo alikataa kuondoka katika gereza maarufu la Kamiti akisema anahofia maisha yake.

Muhubiri huyo alidai kuwa anaweza kutekwa nyara na kuuawa na serikali mara tu atakapokuwa huru.

Hakimu mkuu aliamuru akae gerezani kwa muda usiozidi siku 30 kisha aachiwe huru.

Hata hivyo atalazimika kuilipa serikali kwa kukaa kwake katika kituo hicho.

Bw Buru amewasilisha kesi tofauti katika mahakama kuu akitaka kupata ulinzi wa serikali pindi atakapoachiliwa.

Kesi yake imeibua mjadala kuhusu watu kutoweka nchini Kenya.

Ripoti ya hivi majuzi ya Amnesty International na mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu ililaumu polisi kwa ongezeko la ukatili na mauaji ya kiholela pamoja na utekaji nyara nchini Kenya.

Polisi wamekanusha madai hayo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved