logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Nilipiga nduru za furaha sana!" Boniface Mwangi asherehekea uteuzi wa Karua

Mwangi ameidhinisha serikali ya muungano wa Azimio la Umoja.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri17 May 2022 - 05:26

Muhtasari


•Mwangi amemsifia sana mbunge huyo wa zamani wa Gichugu na kusema kuwa ana rekodi kubwa ya kupigania mabadiliko.

•Mwangi ameonekana kuidhinisha serikali ya muungano wa Azimio la Umoja na kuitaka iwaadhibu wafisadi iwapo itatwaa ushindi.

Mara nyingi mwanaharakati mashuhuri Boniface Mwangi ameonekana kuwapinga na kuwakosoa wanasiasa wa Kenya pamoja na matendo yao.

Mwangi hata hivyo ameonyesha wazi upendelea kwa  kiongozi wa NARC-K Martha Karua na ambaye nimgombea mwenza mteule wa Raila Odinga.

Amefichua kuwa alipokea uteuzi wa Karua kwa shangwe na nderemo tele hadi kupiga hatua ya kuenda nyumbani kwake kumpongeza.

"Nilikuwa kwenye kinyozi alipotangazwa kuwa Naibu Rais aliyeteuliwa, na nilipiga mayowe kwa furaha nyingi. Ilitubidi kwenda nyumbani kwake kumpongeza. Martha ndiye atakayebadilisha mchezo katika uchaguzi huu," Mwangi alisema kupitia Instagram.

Mwanaharakati huyo amemsifia sana mbunge huyo wa zamani wa Gichugu na kusema kuwa ana rekodi kubwa ya kupigania mabadiliko.

Mwangi ameonekana kuidhinisha serikali ya muungano wa Azimio la Umoja na kuitaka iwaadhibu wafisadi iwapo itatwaa ushindi.

"Martha Karua ni  safi, wa kuaminika na mwenye msimamo thabiti. Ana rekodi ya kupigania mabadiliko tangu. Baba amepata mwenza katika Martha. Raila Odinga na Martha Karua sharti wawaahidi Wakenya kwamba wazabuni, wanyakuzi wa ardhi na waporaji watafungwa jela," Alisema.

Kiongozi huyo wa Ukweli Party aliambatanisha ujumbe wake na picha na video zake akiwa na mkewe pamoja na Karua.

Raila alitangaza kiongozi huyo wa Narc Kenya kuwa chaguo lake la mgombea mwenza katika mkutano uliofanyika Jumatatu nje ya ukumbi wa KICC.

Iwapo watashinda kura ya urais katika uchaguzi wa Agosti, Karua atakuwa naibu rais wa kwanza mwanamke nchini Kenya.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved