logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Mlango" wagunduliwa katika sayari ya Mars

Kulingana na NASA, ni suala la kimtazamo.

image
na Radio Jambo

Habari19 May 2022 - 09:13

Muhtasari


•Baadhi wamebaini kuwa ni umbo la "mlango" na wengine wameibuka na nadharia kuhusu iwapo ’’mlango’’ huu uliopo nje ya dunia unaweza kubuni "njia " ya kuingia katika sayari jirani.

Likionekana kama umbo la mraba, na mkato laini unaoonekana katika mwamba mkali, umbo la kijiolojia lililotengenezwa katika sayari ya Mars limeibua maswali kwa siku kadhaa.

Baadhi wamebaini kuwa ni umbo la "mlango" na wengine wameibuka na nadharia kuhusu iwapo ’’mlango’’ huu uliopo nje ya dunia unaweza kubuni "njia " ya kuingia katika sayari jirani.

Lakini kile kilichoonyeshwa ni picha iliyopigwa na roboti ya udadisi, ambayo imekuwa ikituma taarifa kuhusu sayari ya Mars kutoka duniani tangu mwaka 2012, ina maelezo zaidi ya kimantiki.

Kulingana na NASA, ni suala la kimtazamo.

NASA ilitambua picha kama sehemu ya msururu wa "Sol 3466" ambao ulichapishwa katika picha nyingi katika wavuti wa mpango wa uvumbuzi wa roboti

Baada ya kuchapishwa, baadhi ya watu mtandaoni walianza kuzungumzia nadharia kuhusu umbo lake na jinsi umbo hivyo lilivyo na muonekano wa ‘’mlango’’ au "njia"

Katika picha hii unaweza kuona mkusanyiko wa picha za misururu ya 3466 na jinsi umbo linavyoonekana kwenye mwamba wa Jezero , ambalo limevumbuliwa na roboti yenye udadisi katika wiki za hivi karibuni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved