Watu 5 wazikwa wakiwa hai baada ya choo kuporomoka Kiambu

Muhtasari

•Tukio hilo lilitokea baada ya msingi wa choo kuporomoka. Watano hao walikuwa wakijenga choo hicho siku ya Ijumaa,

Watu watano walizikwa wakiwa hai katika Shule ya Sekondari ya Mukua ya PCEA huko Githunguri, Kiambu
Watu watano walizikwa wakiwa hai katika Shule ya Sekondari ya Mukua ya PCEA huko Githunguri, Kiambu
Image: HISANI

Watu watano walizikwa wakiwa hai katika Shule ya Sekondari ya PCEA Mukua iliyo Githunguri, kaunti ya Kiambu.

Tukio hilo lilitokea baada ya msingi wa choo kuporomoka. Watano hao walikuwa wakijenga choo hicho siku ya Ijumaa,

Shughuli ya uokoaji ilianza punde huku watoa huduma za dharura wakifika katika eneo la tukio muda mfupu baadae.

Maafisa wa usalama pia walifika katika eneo la tukio kusaidia katika kurejesha hali ya utulivu huku juhudi za uokoaji zikiendelea.

Hii si mara ya kwanza kwa kaunti ya Kiambu kukumbwa na masaibu yanayohusisha majengo yanayoendelea kujengwa.

Kaunti hiyo imeshuhudia kubomoka kwa majengo kadhaa ya makazi yanayoendelea kujengwa.

Hii imeibua wasiwasi juu ya uwezo wa wale waliopewa kandarasi ya kuunda muundo huo.

Serikali ya kaunti pia imelaumiwa kwa kutoa kibali kwa wahandisi wasio na uwezo ambao huishia kufanya kazi chafu zinazohatarisha maisha ya wakaazi.