Jamaa anayedaiwa kusafirisha misokoto 3,900 ya bangi akamatwa Homa Bay

Muhtasari

•Polisi huko Homa Bay Jumatano walimkamata mshukiwa wa mfanyabiashara wa bangi kutoka lokesheni ndogo ya Kakelo Dudi.

•Kamanda wa Kaunti ya eneo hilo Esther Seroney alikariri kuwa serikali kutovumilia kabisa ulanguzi na umiliki wa dawa za kulevya.

 

Kennedy Odhiambo, mshukiwa wa mfanyabiashara wa bangi alikamatwa na roli 3,900 za bangi mnamo Juni 15,2022. Picha: NPS/Twitter
Kennedy Odhiambo, mshukiwa wa mfanyabiashara wa bangi alikamatwa na roli 3,900 za bangi mnamo Juni 15,2022. Picha: NPS/Twitter
Image: NPS/Twitter

Polisi katika kaunti ya Homa Bay wanamzuilia mshukiwa wa ulanguzi wa mihadarai anayedaiwa kusafirisha zaidi ya misokoto 3900 ya bangi.

Kennedy Odhiambo Oyoo alikamatwa Jumatano katika eneo la Kakelo Dudi kwa kusafirisha baada ya kusakwa kwa muda mrefu.

 Kulingana na Tume ya Kitaifa ya Huduma kwa Polisi, mshukiwa amekuwa akitumia ujanja kuwapita maafisa walionuwia kumkamata. Alinaswa wakati wa oparesheni ya kukabiliana na pombe haramu na dawa za kulevya.

Bangi hiyo ilipatikana katika nyumba yake tarehe tofauti.

Mnamo Oktoba 11, 2021, maafisa walipata misokoto 800 za bangi mjini Homabay. Misokoto hiyo zinadaiwa kuwa za Odhiambo.

Kamanda wa Kaunti ya Homabay Esther Seroney alisisitiza kuwa serikali haitaruhusu ulanguzi na umiliki wa dawa za kulevya katika eneo hilo.

Odhiambo yupo kizuizini akisubiri kufikishwa mahakamani.

"Atafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kwa madhara yote ambayo amesababisha ndani ya jamii yake na kwingineko," NPS ilisema.

Haya yanajiri siku moja baada ya dereva wa lori kukamatwa huko Webuye, Bungoma kwa ulanguzi wa bangi kati ya Kenya na Uganda.

Dereva huyo alikamatwa kwenye barabara ya Webuye-Malaba katika eneo la pan paper akisafirisha magunia 50 ya bangi kutoka Uganda hadi Mombasa.

OCPD wa Webuye Mashariki Martha Ng'etich alisema baada ya ukaguzi wa kitaalamu kutoka kwa Kurugenzi ya Idara ya Upelelezi wa Jinai, ilibainika kuwa thamani ya mitishamba hiyo ilikadiriwa kuwa Sh15 milioni.