Babake marehemu Frank Obegi alizungumza na vyombo vya habari siku moja baada ya mwili wa mwanawe uliokuwa umekatwakatwa kupatikana katika Msitu wa Kijabe pamoja na miili ya wengine watatu.
Babake Obegi, Evans Bowendo, alieleza kwamba alifahamu kuhusu kifo cha mwanawe kupitia kwa mmoja wa marafiki zake. .
Isitoshe, Bw. Bowendo pia na mara zote alidhani aliuza ‘tiketi za ndege’ na kufanya uandishi wa kitaaluma.
“Nilidhani kuwa mwanangu aliuza tikiti za ndege mtandaoni. Hivyo ndivyo alivyokuwa ameniambia alipoondoka nyumbani Februari. Lakini sasa amekutwa amekufa, pia nimeshtuka ni kitu gani kilimfanya mwanangu afe vile.
Alikuwa na pesa. Alipopata pesa ungeona kwenye status yake ya WhatsApp, mara Mombasa, wakati mwingine alikuwa kwenye ndege. Nilimuuliza akaniambia pesa alizonazo huwa ni yake kutokana na biashara aliyokuwa anaifanya'' Bw, Bowedo alisema.
Kaka yake Obegi kwa upande wake aliwaambia waandishi wa habari kwamba kwa sababu marehemu alikuwa mwanablogu maarufu, hakuwahi kutilia shaka chanzo cha mapato yake.
"Alikuwa mtu ambaye alikuwa akifanya kazi kwenye mitandao ya kijamii, alikuwa mwanablogu, na labda alikuwa mahali pasipofaa, kwa wakati mbaya na watu wasiofaa."
Mwili wa marehemu Obegi uliokuwa na ishara za mateso ulipatikana pamoja na miili ya Fred Obare, Elijah Omeka na Moses Nyachae katika Msitu wa Kijabe na eneo la Magadi.
Wanne hao waliishi maisha ya kifahari wakizunguka nchi nzima kupitia ndege na matumizi yao ya kifahari katika vilabu na vituo mbalimbali.