Video: Tazama jinsi rais wa Marekani Joe Biden alivyoanguka kutoka kwa baiskeli

Muhtasari

•Joe Biden alinaswa mguu wake na kuanguka kutoka kwa Baiskeli ambayo alikuwa  anaendesha  katika jimbo la Delaware.

•Baada ya kusimama,Joe Biden aliipanda baiskeli yake tena na kuanza kuiendesha tena, thibitisho kuwa hakuumia vibaya.

Rais wa Marekani, Joe Biden, alinaswa mguu wake na kuanguka kutoka kwa Baiskeli ambayo alikuwa  anaendesha  katika jimbo la Delaware.

Haya yalitokea wakati alikuwa akisherehekea kumbukumbu ya miaka 45 ya harusi yake na Mama wa Kwanza Jill Biden.

Hafla hiyo ilifanyika katika  bustani ya serikali  iliyo karibu na nyumba yake  huko Rehoboth Beach, hii ni  kulingana na Ikulu ya White House.

Katika video iliyosambazwa mtandaoni, rais huyo  alionekana kuamka sekunde chache  tu baada ya kuanguka.

Watu waliokuwa karibu naye walipomuuliza kuhusu hali yake  baada ya kuanguka,Biden alijibu kwa kusema ‘Niko sawa’.

Rais  huyo hakuhitaji matibabu baada ya kuanguka kutoka kwa baiskeli yake .

Baada ya kusimama,Joe Biden aliipanda baiskeli yake tena na kuanza kuiendesha tena, thibitisho kuwa hakuumia vibaya.

Hii sio mara ya kwanza  kwa rais Joe Biden kuanguka chini hadharani. Hapo awali aliwahi kuanguka kutoka kwenye ngazi za ndege ya  Air force 1.

Kuanguka kwa Biden kutoka kwenye baiskeli ilileta mjadala  ya mseto haswa kutoka kwa mpinzani wake wa kisiasa Donald Trump.

Trump ambaye alikuwa akizungumza wakati wa ziara yake ya American Freedom huko Memphis, Tennessee.

''Inashangaza  sana kuona mtu ambaye  amekaa Ikulu kwa muda mingi bado hajui kukuwa rais wa Marekani'' Trump alisema.

Rais huyo wa zamani alisema kuwa hatawahi kuendesha baiskeli kwa sababu anaogopa kuanguka.

''Tunamtakia Biden afueni ya haraka, hilo lilikuwa anguko mbaya''