Dereva wa lori la taka apigwa risasi mara sita kwenye Barabara kuu ya Thika

Muhtasari

•Kisa hicho kilitokea mwendo wa saa 10 jioni katika Barabara kuu ya Thika.

•Polisi na mashahidi walisema mwathiriwa alipigwa risasi angalau mara sita na mtu mwenye bunduki ambaye alikuwa na bunduki aina ya AK47.

Eneo la tukio la uhalifu
Crime Scene Eneo la tukio la uhalifu

Dereva wa lori la kuzoa taka alipigwa risasi Alhamisi usiku  alipokuwa akingojea lori lake kujazwa na taka kwenye barabara ya Thika.

Dereva huyo aliyetambuliwa na wenzake kuwa Maina  ndiye aliyekuwa akiendesha lori lililopewa kandarasi na Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu ya Kenya kukusanya uchafu.

 Kisa hicho kilitokea mwendo wa saa 10 jioni katika Barabara kuu ya Thika.

Polisi na mashahidi walisema mwathiriwa alipigwa risasi angalau mara sita na mtu mwenye bunduki ambaye alikuwa na bunduki aina ya AK47.

Maina alikuwa ameliendesha lori hilo hadi kwenye Mtaro wa Utalii na kuliegesha hapo akingoja takataka zilizokusanywa kujazwa wakati gari la saluni liliposimama nyuma ya lori lake.

Mashahidi walionusurika katika tukio hilo walisema mtu mmoja aliyekuwa na bunduki alitoka kwa gari na kuelekea alipokuwa dereva na kumpiga risasi sita kabla ya kurejea kwenye gari na kuondoka.

Wanaume wengine  sita waliokuwa wakijaza taka kwenye Lori hawakujeruhiwa katika shambulio hilo.

Kikosi cha polisi kilitembelea eneo la tukio na kuwahoji wahudumu wengine ambao walisema walikuwa wamezoa taka kutoka katikati mwa jiji na walikuwa wakielekea Kasarani.

''Gari hilo la Salun lilikuwa limelifuata lori hilo kutoka katikati mwa jiji'' mashahidi walisema.

Mkuu wa polisi wa Starehe William Sirengo alisema bado hawajabaini sababu za shambulio hilo.

Polisi walisema mwili huo ulihamishwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti na kwamba inaonekana nia ya genge hilo ilikuwa kumuondoa marehemu.

Timu ya wapelelezi inachunguza suala hilo.

Kwingineko ni ,mwendeshaji bodaboda alipigwa risasi na kujeruhiwa kabla ya kuibiwa Sh170,000 katika kisa cha eneo la Kayole Nairobi.

Mwathiriwa alikuwa amepewa pesa hizo kutoka kwa duka kubwa la eneo hilo kuipeleka benki hi alipovamiwa na wanaume wawili waliokuwa wakiendesha pikipiki mita chache kutoka benki.

Alipigwa risasi mguuni na mkononi na mtu mmoja kabla ya kunyakua pesa hizo na kuondoka kwa kasi katika tukio la saa saba mchana.

Polisi wanasema bado hawajapata watu hao wenye silaha na wanaamini walikuwa na taarifa za awali kuhusu pesa hizo.