Mwanafunzi wa chuo kikuu afariki kwa kujitoa uhai kwa kukosa alama

Muhtasari

•Polisi walisema waligundua marehemu alikuwa na jeraha la kuchomwa kisu kifuani na alitumia kebo ya laptop kujinyonga.

•Polisi wamewahoji marafiki kadhaa wa marehemu huku wakichunguza kisa hicho. Visa vya kujiua vimeongezeka katika miezi iliyopita.

Kamba ya kujiua
Kamba ya kujiua
Image: Image: Courtesy

Polisi wanachunguza madai ya mwanafunzi wa mwaka wa nne katika Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Kilimo cha Jomo Kenyatta alifariki kwa kujitoa uhai kwa kukosa alama.

Mwili wa mwanafunzi wa mwaka wa nne Lenny Jessy Masiaga, 22 ulipatikana ukining'inia katika chumba chake huko Juja, Kaunti ya Kiambu.

Kisa hicho kilitokea wikendi katika eneo la Maya Apartment kando  mnamo Juni 25 asubuhi. Mwili huo uligunduliwa na mpenzi wake ambaye alikuwa amekwenda kumtembelea.

Polisi walisema waligundua marehemu alikuwa na jeraha la kuchomwa kisu kifuani na alitumia kebo ya laptop kujinyonga.

Polisi wanaoshughulikia suala hilo walisema wanataka kubaini ikiwa mwanafunzi huyo alijiua au aliuawa.

Mpenzi wake wa kike aliwaambia polisi kuwa marehemu alipangiwa kuhitimu Juni 28, wakati taasisi hiyo ikifanya sherehe za mahafali ya 38 lakini aliposhindwa kupata alama zake zote alikasirika.

Hapo ndipo alipojifungia chumbani na kujichoma kisu kifuani kabla ya kujinyonga saa 2 asubuhi.

Polisi waliitwa kwenye eneo la tukio na kuupeleka mwili wa marehemu kwenye chumba cha kuhifadhia maiti ambapo uchunguzi wa maiti ulipangwa kama sehemu ya uchunguzi wa tukio hilo.

Polisi wamewahoji marafiki kadhaa wa marehemu huku wakichunguza kisa hicho. Visa vya kujiua vimeongezeka katika miezi iliyopita.

Polisi walishughulikia kesi 499 mwaka wa 2019 na 575 mwaka wa 2020. Takriban watu 313 wanaripotiwa kujiua kati ya Januari na Julai 2021.