Mwanamuziki Kevin Kioko almaarufu Bahati ambaye pia analenga kiti cha ubunge Mathare kupitia tikiti ya Jubilee amemkosoa vikali katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna kwa matamshi yake kwamba vuguvugu la Azimio lacUmoja limeamua kumuunga mkono Anthony Oluoch wa ODM katika kinyang’anyiro cha ubunge Mathare.
Hata baada ya maamuzi ya Sifuna Bahati akihutubia wanahabari siku ya Jumatatu alisema kwamba hatajiuzulu kwa ajilo ya mtu yeyote.
Bahati ambaye alichukizwa na matakwa hayo ya katibu mkuu wa ODM aliamua kukunja shati na kujibwaga ulingoni katika kutupiana maneno makali na Sifuna huku akimtaka aachane na eneo bunge la Mathare kabisa kama kweli anataka kura za eneo bunge hilo kumvusha kuwa Seneta wa Nairobi.
Mimi nashangaa na huyu Sifuna, 2013 alikuwa na tikiti ya ODM huko Kanduyi na akaanguka, 2017 alikuwa na tikiti ya ODM na bado akaanguka Seneta hapa Nairobi. Na huyu jamaa vile anaendelea kuchezea youth, hana heshima kwa youth, hata huu mwaka tutakuwa tulifanya maamuzi mabaya kama Azimio, ataanguka tena! Sifuna fagia kwako."
Huku mkewe Bahati akimtetea, aliweka mambo wazi kuwa Bahati hatajiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho kwa ajili ya mtu yeyote.
"Kelvin Bahati mbunge wa Matahre ajaye, hatajiondoa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge kwa ajili ya mtu yeyote PERIOD," Aliandika Diana.
Hii sio mara ya kwanza azma ya msanii huyo kukumbwa na matatizo.