Nyama ya matumbo ni kipande cha nyama inayotoka katika tumbo la wanyama wa shamabani kama vile ng'ombe, nguruwe, kondoo na mbuzi.
Tamaduni nyingi kote ulimwenguni zimekuwa zikitumia kwa muda mrefu kama chanzo cha afya cha protini.
Nyama hii inaweza kupatikana katika mikahawa barani Asia, Afrika baadhi ya maeneo ya Amerika na bara Ulaya. Nyama hii ina faida nyingi katika mwili wa bindamau ikilinganishwa na nyama nyengine.
Supu ya utumbo ni kivutio kikubwa miongoni mwa watu wa bara Afrika na wengine huyakaanga na kuyaongezea ladha tamu.
Upande wa kiafya, nyama ya matumbo ina manufaa mengi ikiwemo wingi wa protini na virutubisho vingine ambavyo ni muhimu kwa afya.
Faida ya nyama ya utumbo
Utumbo una vitamini na madini mengine ambayo ni muhimu kwa mwili wetu, na unapoliwa, una virutubishi ambavyo vina faida kwa afya zetu, kulingana na mchambuzi wa afya wa Webmd.com.
Inazuia upungufu wa damu mwilini
Utumbo una vitamini B12, ambayo huzuia upungufu wa damu mwilini , hususan miongoni mwa watu waliochoka na wasioweza kutembea.
Inajenga mifupa na misuli mwilini
Nyama ya utumbo ina protini inayosaidia kujenga misuli na mifupa. Vilevile nyama hiyo ina asidi zote 9 muhimu ambazo mwili wetu unahitaji kufanya kazi, kulingana na Healthline.com.
Imejaa madini na vitamini
Nyama ya utumbo ina virutubisho kama vile madini ya zinki, selenium na kalsiamu. Zinki husaidia watu seli za mfumo wa kinga wa mwili kusaga vyakula vya wanga. Selenium husaidia kuboresha jeni na afya.
Kupunguza uzani
Kula vyakula vyenye protini nyingi husaidia kudhibiti lishe na kupunguza uzito.
Utumbo una viwango vya chini vya Kalori ikilinganishwa na vyakula vingine.
Ulaji wa vyakula vyenye protini nyingi humsaidia mtu kupunguza uzito na kupunguza kiwango cha ulaji wa chakula, kwa mujibu wa Healthline.com.
Hatari ya kuvimbiwa
Nyama ya utumbo ina mafuta mengi ikilinganishwa na nyama nyingine, na watu walio na mafuta mengi mwilini wanaweza kuathiriwa kwa njia tofauti.