Kenya yarejelea mauzo ya miraa nchini Somalia

Somalia ilipiga marufuku miraa kutoka Kenya mnamo mwezi Machi 2020

Muhtasari

•Hii inafuatia kutiwa saini kwa mikataba kadhaa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ikiwa ni pamoja na kuanzisha biashara ya mirungi. (miraa)

•Somalia ilipiga marufuku miraa mnamo mwezi Machi 2020 kufuatia uhusiano mbaya wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Image: BBC

Ndege ya kwanza ya mizigo iliyosafirisha shehena ya mirungi hadi Mogadishu ilipaa mapema Jumapili baada ya kupigwa marufuku kwa miaka miwili.

Hii inafuatia kutiwa saini kwa mikataba kadhaa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ikiwa ni pamoja na kuanzisha biashara ya mirungi ambayo pia inajulikana kama miraa.

Katika makubaliano hayo, Somalia itasafirisha samaki na bidhaa nyingine nchini Kenya.

Habari hizi zitakuwa afueni kubwa kwa wafanyabiashara wa miraa nchini Kenya ambao wameathiriwa na kuzorota kwa biashara ya bidhaa hiyo.

‘’Ahadi yetu kama serikali kusaidia wakulima wa miraa na sekta nyingine zote katika kupata fursa za soko za ndani na kimataifa bado ni thabiti,’’ Peter Munya, Waziri wa Kilimo wa Kenya alisema.

Somalia ilipiga marufuku miraa mnamo mwezi Machi 2020 kufuatia uhusiano mbaya wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Marufuku hiyo ilisababisha hasara ya soko la kila siku la zaidi ya tani 50 za mirungi yenye thamani ya zaidi ya Sh20 milioni (dola 169,296.78) wakati huo.

Tangu Rais Hassan Sheikh Mohamud ambaye alichaguliwa tena mwezi Juni baada ya kupigiwa kura mwaka wa 2017