logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Inspekta wa polisi afariki kwa kujitia kitanzi ndani ya bafu Juja

Afisa huyo alikuwa na kesi ya kushambuliana na alitangazwa kuisusia tangu Desemba 2021.

image
na

Habari29 July 2022 - 03:08

Muhtasari


•Polisi walisema walipigiwa simu na kufahamishwa kuwa inspekta Wilson Mugambi Gitonga alifariki kwa kujitoa uhai.

•Kwingineko jijini Nairobi, mwanamume mmoja alifariki baada ya kuruka kutoka juu ya barabara ya Globe Cinema.

Mwili wa afisa mkuu wa polisi ulipatikana ukining'inia katika bafu yake huko Juja, Kiambu, katika kile kinachoshukiwa kuwa kisa cha kujitoa uhai.

Polisi walisema walipigiwa simu na kufahamishwa kuwa inspekta Wilson Mugambi Gitonga wa kituo cha polisi cha Mitunguu, kaunti ya Meru alifariki kwa kujitoa uhai.

Walipofika nyumbani kwake walimkuta amejitia kitanzi bafuni.

Afisa huyo alikuwa na kesi ya kushambuliana na alitangazwa kuisusia tangu Desemba 2021.

Polisi waliofika eneo la tukio walisema bado hawajaweza kubaini chanzo cha tukio hilo. Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

Kwingineko jijini Nairobi, mwanamume mmoja alifariki baada ya kuruka kutoka juu ya barabara ya Globe Cinema.

Walioshuhudia walisema kuwa mwanamume huyo alikwea ukuta wa barabara hiyo ya juu na kujishikila pale kwa sekunde chache kabla ya kuruka chini karibu mita 20 na kufa papo hapo.

Mwili wake ulihamishwa hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.

Polisi wanasema wanarekodi angalau visa viwili vya watu kujitoa uhai nchini, jambo ambalo linatia wasiwasi.

Polisi walishughulikia kesi 499 mwaka wa 2019 na 575 mwaka wa 2020. Takriban watu 313 wanaripotiwa kujiua kati ya Januari na Julai 2021.

Polisi bado hawajatoa data za mwaka huu ambazo wanasema ni za kutisha.

Ili kukabiliana na tishio hilo, mamlaka zimekuwa zikishinikiza kuwepo kwa kampeni kuhusu afya ya akili katika huduma ya polisi, ambayo ni miongoni mwa zilizoathirika zaidi.

Kama sehemu ya juhudi za kukabiliana na hali hiyo, mamlaka za polisi zimezindua huduma za ushauri nasaha.

Kitengo cha ushauri nasaha, miongoni mwa mambo mengine, kitatathmini, kubuni na kuongoza programu ya kufikia watu ambayo husaidia kuzuia afya ya akili na matumizi mabaya ya dawa za kulevya.

Zaidi ya hayo, itasaidia wateja na familia zilizoathiriwa na afya ya akili, matumizi mabaya ya dawa za kulevya na kiwewe kwa njia za kushinda shida.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved