Rais Uhuru Kenyatta amekanusha madai kwamba aliwafukuza baadhi ya waliokuwa washirika wake kutoka kwa serikali.
Akizungumza Jumapili jioni, mkuu huyo wa nchi alisema hakuwahi kumfukuza mtu yeyote kutoka serikalini.
"Hata wale waliosema handshake ilibadilisha mambo serikalini. Je, kuna mtu yeyote niliyemfukuza kazini? Sijawahi kumfukuza mtu yeyote serikalini," Uhuru alisema.
Haya yanajiri kufuatia matamshi mbalimbali ya naibu wake na mgombea urais wa Kenya Kwanza William Ruto akidai kuwa alifurushwa kutoka serikalini.
DP alisema awali jukumu lake lilikabidhiwa Waziri wa Usalama wa Ndani Fred Matiang'i ambaye aliteuliwa kuwa mwenyekiti na mratibu wa mipango na miradi ya maendeleo ya serikali.
Akizungumza Jumapili usiku na vyombo vya habari, Uhuru alisema mabadiliko pekee yatakuwa kwamba hatakuwa Rais tena na hatakuwa akifanya kazi kutoka Ikulu.
“Hatuendi popote, bado tutafanya kazi pamoja, kazi ni kubwa, nimebakiza kazi moja tu na nitaanza nyingine,” alisema. [07/08, 20:56] Gm na mabadiliko ya uzoefu.