logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Diamond Platnumz atoa wito wa amani kwa Wakenya

Platinumz alitumia ukurasa wake wa Instagram kuwaomba Wakenya kudumisha amani

image
na Radio Jambo

Habari15 August 2022 - 19:20

Muhtasari


  • Mwanamuziki huyo aliwataka Wakenya kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuungana kwa manufaa ya taifa
Msanii Diamond Platnumz ametajwa kuwa mmoja wa watumbuizaji katika hafla ya Azimio Kasarani

Huku baada ya DP Ruto kutangazwwa kuwa rais mteule na tume ya uchaguzi na mipaka siku ya Jumatatu, kupitia kwenye mitandao ya kijamii watu walitoa wito wa amani.

Mwimbaji wa Tanzania, Diamond Platnumz, Jumatatu alituma ujumbe wa pongezi kwa Wakenya kwa kukamilisha kwa amani zoezi la uchaguzi.

Platinumz alitumia ukurasa wake wa Instagram kuwaomba Wakenya kudumisha amani baada ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kumtangaza William Ruto kuwa rais mteule.

Mwanamuziki huyo aliwataka Wakenya kuweka kando tofauti zao za kisiasa na kuungana kwa manufaa ya taifa.

Sasa hivi si Team Ruto, Wajakoya ama Team Odinga, ni Pamoja Team Kenya,Ili kwa pamoja maendeleo ya Kenya na Wana Kenya Kwa Ujumla,” Aliandika Diamond.

Ujumbe wake Diamond unajiri baada ya viongozi wa kidini NCCK kuwaomba wakenya wadumishe amani wakati huu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved