Rais mteule William Ruto siku ya Jumanne, alipokea ujumbe wa kheri njema kutoka Serbia. Ujumbe huo uliwasilishwa kwa rais mteule na balozi wa Serbia Dragan Zupanjevac katika makazi yake rasmi mtaani Karen.
Kwenye taarifa, Rais mteule aliishukuru Serbia kwa ushirikiano wake na nchi hii,akisema ataweka mikakati kuimarisha hata zaidi ushirikiano katika Nyanja za kilimo,teknolojia na afya.
Ruto ameendelea kupokea risala za pongezi kutoka kwa viongozi mbali mbali tangu alipotangazwa kuwa mshindi kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe tisa mwezi huu na tume ya uchaguzi.
Ushindi wake hata hivyo umepingwa,huku rufaa tisa zikiwasilishwa katika mahakama ya upeo,ikiwemo ile ya Azimio la Umoja-One Kenya.
"Tunakaribisha hamu kubwa ya Serbia ya kufanya kazi na utawala wetu. Tunajitolea kuimarisha uhusiano wetu na kuongeza maeneo ya ushirikiano kama vile kilimo, Teknolojia ya Habari na huduma ya afya," aliandika Ruto.