logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kama Freemason ni mabingwa wa hisani, umejenga shule ngapi? - Miguna amuuliza Rachier

Ikiwa FREEMASONS ni mabingwa wa hisani, je wamejenga shule ngapi, hospitali, vituo vya watoto yatima na walala hoi? - Miguna.

image
na Davis Ojiambo

Habari03 October 2022 - 11:45

Muhtasari


  • • Rachier alikuwa amefunguka kuwa kundi la Freemason ambalo yeye ni mwanachama wa muda mrefu ni mabingwa wa hisani katika jamii.
  • • Miguna alitaka kujua kama kweli ni wahisani basi Rachier amefadhili masomo ya watoto wangapi Kenya.
Miguna amzomea Rachier kwa kutetea kundi la Freemason kuwa ni mabingwa wa kufanya hisani katika jamii.

Wikendi iliyopita, mwenyekiti wa klabu cha soka cha Gor Mahia Ambrose Rachier alikuwa gumzo kubwa baada ya kufichua kwamba amekuwa kwenye kundi linalohusishwa na ushirikina wa kishetani, Freemason.

Kufuatia kufunguka huko, watu mbali mbali wamemjia juu kuuliza maswali kuhusu kundi hilo haswa pale aliposema kuwa azimio lao kuu ni kufanya hisani katika jamii.

Rachier alikanusha dhana inayohusisha kundi hilo na kuwapa watu utajiri pindi wanapojiunga nao na kusema kwamba wanachokifanya ni ihsani tu ili kuwakimu kimaisha wanachama wake.

Matamshi haya ndiyo yamemfanya wakili aliye uhamishoni Miguna Miguna kucharuka na kumzomea vikali Rachier kwa kusema kwamba yeye mwenyewe anatoka katika kijiji chenye kimerambwa na umaskini mbele nyuma, juu chini.

Miguna Miguna aliuliza maswali kuwa iwapo ni kweli Freemason inafanya hisani kwa watu, mbona basi haijasaidia watu kukwepa umaskini katika kijiji cha Rachier ambaye ni mwanachama wao kwa miaka 28.

Pia aliraka kujua hiyo hisani imemfanya Rachier kujenga shule au hata hospitali ngapi katika eneo la kijiji chake huko Siaya kama kweli dhumni kuu la Freemason ni kucheza katika nafasi ya msamaria mwema katika uwanja wa maisha.

“Ambrose Rachier anatoka katika eneo la Gem maskini katika Kaunti ya Siaya. Ikiwa FREEMASONS ni mabingwa wa hisani, je wamejenga shule ngapi, hospitali, vituo vya watoto yatima na walala hoi? Rachier amefadhili masomo kwa watu wangapi? ALIUA Gor Mahia kwa ibada yake ya shetani,” wakili Miguna Miguna alitupa bomu la moto kwenye kichwa cha  Rachier.

Awali pia mshirika mwenza katika kampuni ya mawakili ya Rachier & Amollo Advocates, mbunge wa Rarieda Otiende Amollo alijitenga na uwezekano wake kuwa katika Freemason na Rachier.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved