logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ruto kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu Ongata Rongai

Ruto alitangaza kuwa serikali yake itaanzisha nyumba 500,000 za bei nafuu kote nchini.

image
na Davis Ojiambo

Habari18 October 2022 - 08:52

Muhtasari


  • • Nyumba hizo ambazo zimejengwa katika mandhari tulivu ni moja wapo wa miradi ya Boma Yangu ambao ajenda yake kuu ni kutoa nyumba za bei nafuu kwa Wakenya wa mapato ya chini. 

Rais William Ruto leo Jumanne atakagua mradi wa Kings Serenity Affordable Housing Programme, ambao unalenga kujenga ujenzi wa nyumba za bei nafuu katika mtaa wa Ongata Rongai. 

Mradi huo ni wa aina yake huko Rongai. Nyumba hizo ni za vyumba viwili vya kulala. 

Nyumba hizo ambazo zimejengwa katika mandhari tulivu ni moja wapo wa miradi ya Boma Yangu ambao ajenda yake kuu ni kutoa nyumba za bei nafuu kwa Wakenya wa mapato ya chini. 

Mapema mwezi huu, Ruto alisema Serikali itaboresha mpango wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu ili kuwezesha watu wa mapato ya chini kumiliki nyumba. 

Kiongozi huyo wa taifa alisema atashirikiana na wabunge kutafuta njia mwafaka zaidi ya kufanikisha mpango wa nyumba za bei nafuu. 

Alipokuwa akikagua mradi unaoendelea wa nyumba za bei nafuu mjini Nairobi, Ruto alitangaza kuwa serikali yake itaanzisha nyumba 500,000 za bei nafuu kote nchini.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved