Baada ya wakili Miguna Miguna kurejea nchini kutoka Kanada, baadhi ya wafuasi Rais William Ruto wameonekana kupendezwa na hatua hiyo huku wakimtumia jumbe za kumkaribisha nchini.
Kurejea kwa Miguna Miguna kuliwezeshwa na rais William Ruto na washirika wake wa karibu.
Leo Oscar Sudi amesema kuwa,kama mrengo wa kwenye kwanza hawatalipiza kisasi kwa watu waliwadhulumu na kuwatesa.
Maneno yake Sudi yanajiri saa chache baada ya kukutana na waziri Miguna Miguna.
"Uhuru umefika. Hatutalipiza kisasi kwa yeyote aliyetudhulumu. Karibu nyumbani Jenerali @MigunaMiguna."
Usemi wake Oscar Sudi ni kinyume na kile rais William Ruto anafanya na DCI. Kuitwa kwa maafisa kunasikika kama kulipiza kisasi hati za serikali iliyopita. Naam Oscar Sudi ameweka wazi kuwa watasamehe kila mtu.
Baada ya kuwasili nchini mnamo Octoba 20, wakili Miguna Miguna ameanza kufunguka kuhusu masuala kadhaa ambayo yalisababisha kufurushwa kwake nchini na jinsi uhusiano wake na kinara wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga ulivyozorota, licha ya kuwa mwandani wake na hata kumwapisha kama rais wa wananchi.
Freedom is here. We will not revenge to anyone who mistreated us. Welcome home General @MigunaMiguna pic.twitter.com/oMorQXTukC
— Hon Oscar Sudi (@HonOscarSudi) October 22, 2022
Akizungumza katika runinga ya NTV na mwanahabari Joe Ageyo, Miguna alisema kwamba yeye alimpigia Uhuru Kenyatta kura katika uchaguzi wa mwaka 2017 lakini baadae aligundua kuwa Raila alishinda na ndio maana alikuwa mstari wa mbele katika kumwapisha.
Miguna alieleza kuwa kutokana na data alizokuwa nazo, Raila alikuwa ameshinda kura za urais za Agosti 2017. Alisema licha ya kuzozana na waziri mkuu huyo wa zamani na kumchukia, aliamini kuwa angemshinda rais wa wakati huo Uhuru Kenyatta.