Tajiri kutoka kaunti ya Uasin Gishu ambaye pia ni mwanasiasa Zedekiah Bundotich almaarufu Buzeki amewashabikia watu wa kaunti hiyo kwa ujumbe maalumu, miezi miwili baada ya kukamilika kwa mchakato wa upigaji kura.
Buzeki ambaye kwa mara kadhaa amekuwa akijaribu kuwania ugavana wa kaunti hiyo bila mafanikio aliwashabikia wakaazi wa kaunti hiyo kwa kusimama na yeye kipindi cha upigaji kura hata kama hakufanikiwa kuibuka mshindi.
Katika ujumbe maalum alioandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, Buzeki aliwaambia wana Uasin Gishu kwamba hata kama alipoteza kura zao lakini ana uhakika alishinda mapenzi yao kwake.
“Watu wa kupendeza wa Uasin Gishu. Leo, ninawatafakari watu wetu wema. Walinikaribisha kila mara kwa nyimbo tamu na kuniongezea mashujaa wetu maziwa ya Mursik. Walicheza nami na hata kunikaribisha nyumbani kwao. Walisikiliza mipango yangu na hata kufungua mioyo yao ya ndani. Wanawatakia watoto wao mema. Mara nyingi, hawakuwahi kuwasilisha changamoto zao za kibinafsi kwangu lakini wito wa kutia saini katika mwingiliano wetu wote ulikuwa "Soru Lagook" (kuunda fursa kwa watoto wao)” Bundotich alikumbuka.
Vile vile, mwanasiasa huyo mkwasi aliwaahidi watu wa kaunti hiyo kuwa hatowasahau kamwe kwani kama nafasi itatokea huku mbeleni bila shaka atajitokeza kuwahudumia, akiashiria kutokufa moyo katika azma yake ya kuwahudumia katika wadhifa wa kisiasa wakati mmoja majaaliwa.
“Mungu awabariki watu wapendwa, Mungu Mwenyezi atawajaza haja za mioyo yenu. Tayari ninawakosa. Ninaweza kuwa nimepoteza kura, lakini nilishinda upendo wanu. Viongozi mliowachagua wawajibu mahitaji yenu. Nitakuwambuka daima katika maombi na ikitokea fursa nitawatafuta,” Buzeki alimaza kwa ujumbe huo wenye hisia za mapenzi ya kweli.