Mchanganuzi mashuhuri wa kisiasa Mutahi Ngunyi amejitokeza kwa ujasiri kumshauri Winnie Odinga kuchukua nafasi ya kumwambia kwamba nasaba hazirithiwi bali ni za kunyakuliwa.
Kupitia akaunti yake rasmi ya Twitter, Ngunyi amesema;
"Familia ya Odinga imewekeza miaka 100 kujenga nasaba ya kisiasa. Winnie Odinga lazima arithi. Kumbuka kwamba nasaba ni taasisi zenye wivu. Lakini Winnie lazima pia ajue kwamba: Nasaba hazirithiwi, zinachukuliwa. hivi ndivyo Ruto alivyowafanyia Uhuru na Moi."
Winnie ni mwanawe kinara wa chama cha ODM,Raila Odinga na ambaye amekuwa naye katika sako kwa bako.
Winnie anaonekana kufuata nyayo za baba yake ambaye, ni mwanasiasa mashuhuri nchini.
Siku chache zilizopita Winnie alivuma sana mitandaoni baada ya kurejea kwenye mitandao ya kijamii ya Twitter, hii ni baada yake kutoka Twitter mwei mmoja uliopita.
Hivi majuzi habari zilienea kwenye mitandao ya kijamii kuwa Winnie Odinga alikuwa kwenye orodha iliyopendekezwa kwa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Winnie aliwea wazi kwamba hayuko tayari kupokea au kwa nafasi ya EALA.